MTANGAZAJI ALIYEDAIWA KUPOTEA APATIKANA KITUNDA KWA SHANGAZI YAKE

***

Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime amesema Mtangazaji wa TV 3, Gwamaka Francis Gehas, mkazi wa Mbezi Beach African, Dar es Salaam aliyedaiwa kupotea Januari 3, 2025 amepatikana akiwa kwa shangazi yake Kitunda Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa yake Misime iliyotolewa jana Januari 5, Makao Makuu ya Polisi Dodoma, imebainisha kuwa baada ya ufuatiliaji ulioanza kwa kukusanya ushahidi na taarifa kutoka kwa watu mbalimbali, walipokea taarifa kuwa Gwamaka yupo Kitunda nyumbani kwa shangazi yake.

Aidha, Jeshi la Polisi limesema linaendelea na uchunguzi, ikiwa ni pamoja na kupata maelezo yake ili kujua uhalisia wa tukio la kutokuonekana kwake na baadaye kuonekana akiwa kwa shangazi yake.
 

0/Post a Comment/Comments