Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeandaa mafunzo kwa
mawakili wote wa serikali nchini yatakayofanyika kwa siku tano mkoani Arusha
kuanzia Machi 24 mpaka 28 ambayo yatalenga kuongeza umahiri wa utendaji kazi
kwa mawakili hao ambapo Mafunzo hayo yanatarajiwa kushirikisha takribani
mawakili 300.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema hayo leo
Machi 19 wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuelekea mafunzo hayo
yatakayotolewa na wanasheria wabobezi kutoka ndani na nje ya nchi.
Aamesema lengo la mafunzo ni kuboresha utendaji kazi,
kutafuta mwarobaoini wa usuluhishi wa migogoro ya kibiashara, kuongeza ujuzi wa
uandishi wa sheria na mchakato mzima wa kutunga sheria pamoja na kuwaelekeza
mawakili hao kuwa na uzalendo na kulinda maslahi ya Taifa.
“Mafunzo haya yataendeshwa na wanasheria wabobezi wa ndani
na nje ya Jamhuri wa Muungano ya Tanzania katika mada tofauti eneo la kwanza ni
eneo ambalo Rais amekuwa akisisitiza kila siku katika kuimarisha uwezo wetu
katika uandishi, uingiaji na majadiliano ya mikataba mbalimbali ya kimataifa au
hata ile ambayo si ya kimataifa.
“Sasa nini hasa misingi ya mikataba hii na unahitaji kuwa na
ujuzi gani maalumu katika meza ya majadiliano na nini ni miiko ni ipi na
vitu gani unaweza kufanya na vitu gani unaweza usifanye” amesema Johari.
Aidha ametoa wito kwa mawakili wote wa serikali ambao
hawajajisajili kupata mafunzo hayo jisajili mara moja kwa kuwa yataleta tija
katika sekta ya sheria.
Post a Comment