WADAU WATAKIWA KUZITUMIA KWA USAHIHI TAARIFA ZA HALI YA HEWA

Afisa Mwandamizi ICPAC ambaye ni Mtaalamu anayesimamia nchi kumi na moja Afrika anayeangalia matumizi ya taarifa za hali ya hewa Collision Lore akizungumza katika warsha ya siku tano iliyoandaliwa na kituo cha Utabiri wa Hali ya Hewa na Maombi cha IGAD (ICPAC) inayofanyika katika Kaunti ya Nakuru,Mji wa Naivasha Mkoani Kenya,
..................

NA MUSSA KHALID NAIVASHA,KENYA

Jumla ya washikadau kutoka sekta mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari kutoka mataifa manne ya Afrika Mashariki wamekutanishwa nchini Kenya kwa lengo la kujadili umuhimu wa hali ya hewa na utekelezaji katika kuzuia hatari na majanga yanayoweza kutokea.

Akizungumza kwenye warsha ya siku tano iliyoandaliwa na kituo cha Utabiri wa Hali ya Hewa na Maombi cha IGAD (ICPAC) inayofanyika katika Kaunti ya Nakuru,Mji wa Naivasha Mkoani Kenya,Afisa Mwandamizi ICPAC ambaye ni Mtaalamu anayesimamia nchi kumi na moja Afrika anayeangalia matumizi ya taarifa za hali ya hewa Collision Lore amezitaja nchi shiriki kuwa ni pamoja na Kenya,Uganda,Rwanda pamoja na Tanzania.

Lore amesema kuwa kwa sasa watu wanapokea htaarifa za hewa lakini hawazitumiaa inavyotakiwa kwa kutoamini au kuamini hivyo ameeleza ni muhimu kwa wadau wote kushirikiana katika kuzitua taarifa hizo kwa faida katika kuisaidia jamii.

‘Changamoto kubwa inayotukuta sasa tunapeana taarifa za hali ya hewa lakini uelewa kikamilifu bado haujaifiki ipasavyo katika ngazi za mashinani kwani bado wananchi hawajapata uelewa kwa kuzitumia habari hizo kikamilifu katika shughuli zao’amesema Lore

Lore ametumia fursa hiyo kusisitiza wadau kufanya kazi kwa pamoja ikiwemo kutoa elimu ya matazamio ya hali ya hewa ili ujumbe huo uweze kuwafikia watu wanaohusika ili waweze kujikinga na madhara ya mara kwa mara.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Kenya Mwai Zakari amesema kuwa wataendelea kushirikana na wadau mbalimbali ili waweze kufahamu matumizi sahihi ya utabiri wa kila siku,wiki mpaka mwezi uweze kuwasaidia katika shughuli zao.

Meneja wa ofisi kuu ya Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Kantamla Mafuru amesema kutokana na kujifunza teknolojia mpya kwenye mafunzo hayo yatasaidia kuwaongezea ujuzi kwenda kuchakata vizuri mifumo ya hali ya hewa kuweza kujua matukio ya hali ya hewa ili kuijuza jamii matukio yanayoweza kujitokeza.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki katika hafla hiyo akiwemo Mwakilishi kutoka mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria Tanzania (Wizara ya Afya) Dr Sijenunu Aroni amesema amejifunzo namna mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kuathiri kuongezeka au kupungua kwa magonjwa hivyo inasaidia pia sekta ya afya kuweza kujipanga kabla madhara hayajatokea.

Naye Mwakilishi kutoka Wizara ya Maji Tanzania Martin Omego amesema mafunzo hayo yanasaidia kuonyesha mwanga kwa namna ambavyo wanavyofanya shughuli za kila kwa kutumia taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa.

Warsha hiyo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali imeanza kufanyika leo tar 08 -12 Disemba mwaka huu ambapo pia imetajwa kuwa ni itaendelea kufanyika Afrika ambapo itawakutanisha kwa pamoja  Mataifa ya Ethiopia,Somalia,Sudan na Djibout.

0/Post a Comment/Comments