NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA AUSTRIA AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

*****
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Austria anayeshughulikia masuala ya kisiasa, Mheshimiwa Balozi Dkt. Hannah Liko, amewasili nchini Machi 22, 2026 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu inayolenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, biashara na ushirikiano katika maeneo mbalimbali kati ya Tanzania na Austria.

Akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dkt. Liko amepokelewa na Balozi na Mwakilishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Vienna, Mhe. Naimi S. Aziz, pamoja na Balozi wa Austria nchini, mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Dkt. Christian Fellner.

Wakati wa ziara hiyo, Dkt. Liko anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe (Mb.), pamoja na viongozi kutoka wizara mbalimbali zikiwemo Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Wizara ya Fedha, Wizara ya Mambo ya Ndani na Wizara ya Viwanda na Biashara.

Aidha, anatarajiwa kutembelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika nyanja za kitaaluma na elimu ya juu. Ziara hiyo inatarajiwa kuhitimishwa Machi 25, 2026.













 

0/Post a Comment/Comments