SERIKALI ya Tanzania na Belarus zimesaini makubaliano ya kuanzisha kamati ya pamoja ya uchumi na biashara, yakilenga kuimarisha ushirikiano.
Hati hiyo imetiwa saini Aprili 29, 2026 jijini Dar es Salaam kati ya Profesa Kitila Mkumbo na Maxim Ryzhenkov.
Profesa Mkumbo amesema hatua hiyo inalenga kufufua uhusiano wa muda mrefu uliodumaa kwa takribani miongo mitatu.
Ameeleza kuwa makubaliano hayo yatafungua milango ya uwekezaji katika sekta muhimu kama kilimo, viwanda na biashara.
Aidha, amesema ushirikiano huo utaongeza ajira na kusaidia kukuza uchumi wa taifa kupitia teknolojia mpya.
Kwa upande wake, Ryzhenkov ameielezea Tanzania kama mshirika muhimu wa kibiashara katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Amesema nchi yake iko tayari kuwekeza na kushirikiana katika miradi itakayochochea biashara na maendeleo ya pande zote.









Post a Comment