MALIASILI YAIBUKA NA MEDALI MBILI ZA DHAHABU SHIMIWI 2026

......

Na Sixmund Begashe, Moshi 

MALIASILI Sports Club, chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, imezidi kuwashangaza mashabiki zake kutokana na ubora wa hali ya juu wa wachezaji wake, kutokana na kufanya vizuri kwenye mchezo wa mbio mbalimbali. 

Maajabu zaidi ya Wizara hiyo yameoneshwa na mkimbiaji wa kike Bi. Naomi Mgumba, aliyeshika nafasi ya kwanza mita 3,000 kwa dakika 12:22:87 na kuibuka tena mshindi katika mita 800. 

Bi Mgumba ambaye ameshiriki kwa mara kwanza mashindano makubwa ya riadha nchini, amekuwa gumzo kubwa kwa walimu na waamuzi wa kimataifa wa mchezo huo waliopo kwenye michezo ya SHIMIWI inayofanyika kwenye uwanja wa Ushirika Moshi, Kilimanjaro. 

Akizungumza na wakimbiaji hao, Bw. Elia Mtalemwa pamoja na kuwapongeza kwa kazi nzuri ya kuipatia heshma Wizara ya Maliasili na Utalii, amewataka waongeze juhudi ili washinde michezo yote iliyobaki. 

Naye Mwalimu wa timu ya Riadha Maliasili Bw. Elibariki Buko emeendelea kuupongeza uongozi wa Wizara hiyo kwa kuiunga mkono timu hiyo hatua inayotia chachu timu hiyo kushinda kila wakati na kuongeza kuwa wanatarajia kuongeza medali zaidi.

"Huyu mtoto (Bi Mgumba) hakimbiii bali anafyatuka, yaani nilimwona kama hataki vile lakini kwenye kumalizia ametushangaza," alisema Mama Kileo wa Moshi Mjini.

Pamoja na medali mbili za dhahabu, timu hiyo ya Wizara yenye kazi adhimu ya Uhifadhi na Utalii wakimbiaji wanaume wamefanikiwa kuingia falinali kwenye mbio za Mita 100, Mita 800 na Mita 100 mbili za kupokezana vijiti.




 

0/Post a Comment/Comments