TUZO ZA REGGAE NCHINI 'KRMA III',WASHINDI KWENDA UJERUMANI,WASANII WAHAMASISHWA KUSHIRIKI

Mwakilishi kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Abel Ndaga akizungumza katika Mkutano wa waandishi wa habari ambao umefanyika katika Ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa Basata (BASATA) wakati wa utambulisho wa Tuzo za Muziki wa Reggae  za KMCC Reggae Music Awards (KRMA III) zinazotarajiwa kufanyika Julai mosi mwaka huu.[/caption] Mratibu wa Taasisi ya Kukaye Moto Culture Center (KMCC-Tanzania) Diana Martin akitambulisha Tuzo za Muziki wa Reggae  za KMCC Reggae Music Awards (KRMA III) zinazotarajiwa kufanyika Julai mosi mwaka huu katika Mkutano wa waandishi wa habari ambao umefanyika katika Ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa Basata (BASATA). Mwenyekiti wa Kamati ya tuzo za KRMA III Innocent Nganyagwa maarufu Ras Inno akielezea mbele ya  Mkutano wa waandishi wa habari ambao umefanyika katika Ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa Basata (BASATA)  vipengele mbalimbali vitakavyokuwepo kwenye kinyang’anyiro cha Tuzo za Muziki wa Reggae  za KMCC Reggae Music Awards (KRMA III) zinazotarajiwa kufanyika Julai mosi mwaka huu. Mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa Reggae na Dancehall (BOREDA) Grant Cosmas maarufu kama Sukuma Di Push katika Mkutano wa waandishi wa habari ambao umefanyika katika Ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa Basata (BASATA) ameeleza namna watakavyoshirikiana na Taasisi ya KMCC katika  kuelekea kwenye Tuzo za Muziki wa Reggae  za KMCC Reggae Music Awards (KRMA III) zinazotarajiwa kufanyika Julai mosi mwaka huu. Mwenyekiti wa Taasisi ya Rastafari United Front Ras Mabondo Makonnen akizungumza katika Mkutano wa waandishi wa habari ambao umefanyika katika Ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa Basata (BASATA) amesisitiza Umoja na upendo kwa jamii ya Rasta ikiwemo kuonyesha ushirikiano katika Tuzo za Muziki wa Reggae  za KMCC Reggae Music Awards (KRMA III) zinazotarajiwa kufanyika Julai mosi mwaka huu.

Wanakamati wa Tuzo za KRMA III wakisikiliza kwa makini mwenendo wa Tuzo katika Mkutano wa waandishi wa habari ambao umefanyika katika Ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa Basata (BASATA). (picha na Mussa Khalid)

.............................

NA MUSSA KHALID 

Wanamuziki wa Reggae nchini na Maeneo ya Ukanda ndani ya Bara Afrika  wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Tuzo za Muziki wa Reggae  za KMCC Reggae Music Awards (KRMA III) zinazotarajiwa kufanyika Julai mosi mwaka huu.

Akizungumza wakati wa utambulizo wa ujio wa Tuzo hizo kwa waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mwakilishi kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Abel Ndaga ameipongeza Taasisi ya KMCC kwa kuandaa Tuzo hizo kwani zitaendelea kuongeza hamasa kwa wasaini nchini wa Reggae nchini hivyo kukuza Muziki huo.

Aidha amevitaka vyombo vya habari na  wadau mbalimbali Nchini wakiwemo wanamuziki wa Reggae kuonyesha ushirikiano katika kuhamasika kushiriki katika mchakato huo ikiwemo kushirikisha kazi zao za muziki ili ziweze kushindanishwa na hatimaye kujipatia zawadi.

"Sisi kama BASATA tutaendelea kuwaunga mkono wasanii na taasisi mbalimbali katika mipango yao mbalimbali wanayoipanga kwa lengo la kukuza vipaji vya wasanii nchini"amesema Ndaga

Akitambulisha ujio wa Tuzo hizo  Mratibu wa Taasisi ya Kukaye Moto Culture Center (KMCC-Tanzania) Diana Martin amesema kuwa Tuzo hizo ni miongoni mwa miradi ya KMCC ambazo mwaka huu zinafanyika kwa mara ya Tatu ukiwa ni msimu ulioboreshwa zaidi.

Diana amesema kuwa Tuzo hizo zimelenga kutambua mchango adhimu wa muziki wa Reggae kwa jamii na mchango muhimu kwa wanamuziki wa Mtindo huu hapa nchini ili kuwahamasisha kwa kutambua na kuthamini wanachokifanya.

"Tuzo hizi zinaongozwa na mchakato ulioundwa na Kamati ya Weledi zimezingatia ithibati ya Mamlaka simamizi (BASATA),COSOTA na kushirikisha washiriki na wadau kupitia Taasisi zao (BOREDA & RUF) katika hatua za mchakato Ili kuwa na ushirikishanaji Jumuishi utakaojenga ushirikiano miongoni mwa Wana-Reggae nchini"amesema Diana

Aidha kuhusu Mchakato,Diana amesema kuwa ulianza rasmi Januari 27 ambapo unatarajiwa kukamilika Juni 30 kilele cha Usiku wa utoaji Tuzo husika Kuamkia siku ya maadhimisho ya Reggae Duniani Julai Mosi.

Diana amesema kuwa katika Tuzo hizo vipengele mbalimbali vya Muziki wa Reggae visivyopungua thelathini na mojavitatuzwa zikiwemo kazi (Nyimbo) Bora na wasaini waliofanya vizuri zaidi mwaka 2023 kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya tuzo za KRMA III Innocent Nganyagwa maarufu Ras Inno ametaja mchakato wa huo kuwa umezingatia zaidi ya vipengele 30 vitahusika ambapo pia utafanyika uchakataji wa kazi pamoja na upatikanaji wa wateule.

‘Matarajio yetu ni Ushiriki wa Wasanii wa Reggae na kuwa na mwamko wa Hadhira kushiriki sambamba na hatua ya awali ya kusadifisha Muundo (KRMA IV na kuendelea)’amesema Ras Inno

Amevitaja vipengele mbalimbali vitakavyoshindaniwa kuwa ni pamoja na Mwanamuziki Bora wa Kiume wa Dancehall wa Mwaka, Mwanamuziki Bora wa Kike wa Dancehall wa Mwaka, Mwanamuziki Bora wa Kiume wa Reggae wa Mwaka, Mwanamuziki Bora wa Kike wa Reggae wa Mwaka, Wimbo Bora wa Reggae wa Mwaka, Wimbo Bora wa Dancehall wa Mwaka, Mwanamuziki Bora wa Reggae/Dancehall wa Kiume wa Mwaka Anayechipukia, Mwanamuziki Bora wa Reggae/Dancehall wa Kike wa Mwaka Anayechipukia, Wimbo Bora wa Kushirikisha/Kushirikiana wa Reggae/Dancehall wa Mwaka, na Mnenguaji Bora wa Video wa Kiume wa Dancehall wa Mwaka:

Pia amevitaja vipengele vingine kuwa ni Albamu Bora ya Reggae ya Mwaka, Video Bora ya Reggae ya Mwaka, Mtunzi Bora wa Reggae wa Mwaka, Mtunzi Bora wa Dancehall wa Mwaka, Mwanamuziki Bora wa Reggae/Dancehall wa Ukanda wa Afrika Mashariki, Mwanamuziki Bora Dancehall/Reggae wa Ukanda wa Afrika ya Kusini, Mwanamuziki Bora wa Reggae/Dancehall wa Kaskazini mwa Afrika.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa Reggae na Dancehall (BOREDA) Grant Cosmas maarufu kama Sukuma Di Push amesema watahakikisha wanakuwa bega kwa bega na KMCC katika Tuzo hizo ili ziweze kuwa na ukubwa zaidi tofauti na ilivyokuwa huko nyuma.

Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Rastafari United Front Ras Mabondo Makonnen ameendelea kusisitiza Umoja na upendo kwa jamii ya Rasta huku akielezea kuwa ujio wa Tuzo hizo utasaidia kuongeza wigo wa kukuza mawanda ya Muziki huo hapa nchini.

0/Post a Comment/Comments