ANASWA TUHUMA ZA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA 4

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro

..................................

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia mtu mmoja mwenye umri wa miaka 16 (jina limehifadhiwa) kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa miaka 4 ambaye baadaye alipoteza maisha. 

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro akizungumza mapema leo amesema kuwa tukio hilo lililotokea siku ya tarehe 10/11/2021 majira ya saa tatu asubuhi maeneo ya Chamazi Mbande Wilaya ya Temeke.

Aidha, Kamanda Muliro amesema uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo unafanyika na hatua za kisheria wakati wa uchunguzi zitazingatiwa ili haki itendeke.

0/Post a Comment/Comments