Rais wa Zanzibar Mhe.Dkt Hussein Ali Mwinyi akikata utepe Kwenye Uzinduzi wa tawi jipya la huduma za benki ya kiislam crdb Al Barakah huku akiwasisitiza wananchi kuchangamkia fursa zinazotolewa na Benki hiyo.
*****************************************
BENKI ya Crdb yaipongeza Shirika la Zanzibar (ZIC) kwa kuwa Washirika wake wazuri katika huduma miamala ya bima.
Akizungumza na wadau,Masharika, Taasisi mbalimbali zilizojitokeza katika uzinduzi wa Tawi la huduma za benki ya kiislam visiwani Zanzibar Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Crdb Abdulmajid Mussa Nsekela ametaja baadhi ya Taasisi,Masharika kuwa na ushirikiano mzuri wa kuiunga mkono benki hiyo ya kiislam na huduma za kibenki.
"Kupitia benki yetu imeweza kufanya Makusanyo Mazuri ya kifedha kufikia dola za kimarekani milioni 57".
Hata hivyo ametoa pongezi kwa Wizara ya Afya ambapo imekua ikishirikiana kusaidia kukusanya vipimo vya ugonjwa wa uviko ,Shirika la bandari kupitia ukusanywajwi wa ushuru pamoja na Shirika la bima (ZIC) kupitia ukusanywajwi wa mapato kwa njia ya benki .
"Katika jitihada zetu za kuongeza ujumuishi wa kifedha nchini, Benki yetu leo imezindua huduma za kibenki zinazozingatia misingi ya kiislamu “CRDB Al Barakah”, uzinduzi ambao ulienda sambamba na ufunguzi wa tawi letu jipya Zanzibar lilipo Michenzani Mall."
Aidha,Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi. Dkt. Mwinyi ameipongeza benki kwa kuanzisha huduma hizo huku akiwataka wananchi kuchangamkia fursa zinazotolewa kupitia CRDB Al Barakah kujiletea maendeleo.
Post a Comment