JUKWAA LA STB WITH AUSTAR MASAKI KUFANYIKA NOVEMBA 27




*****************************************

Na Mwandishi wetu


MBUNIFU wa mavazi nchini Augustar Masaki, amendaa onyesho la mavazi  Start Tairoling Business with Augusta Masaki, maarufu kama (STB) kwa wabunifu na wanamitindo wachanga ambao walikuwa akiwapatia mafunzo ya ubunifu kwa muda wa miezi mitatu.


Onyesho hilo litakalofanyika Musiam Makumbusho ya Taifa Novemba 27 mwaka huu katika ukumbi wa Makumbusho ya Posta jijini Dar es Salaam. 


Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam, Muandaaji wa jukwaa hilo, Augustar amesema kuwa nguo zitakazo onyeshwa zimetengenezwa na wanafunzi wake wakiwepo walemavu ambao amekua akiwapatia mafunzo na kuvaliwa na wanamitindo wachanga.


"Nimekuwa na darasa kwa vijana ambao wanapenda kuwa wabunifu,  huu ni msimu wa nne mafunzo tunafanya kila mwaka ni bure bila malipo na mwaka huu tumeweza kupata nafasi ya kushirikiana na wabunifu walemavu ambao tutashirikiana nao katika kuonyesha mavazi katika jukwaa la Stb."


Mavazi ambayo yataonyeshwa yametengenezwa na wahitimu ambao pia tutawatunukia vyeti vyao, na zawadi kwa watakaofanya vizuri zaidi niwakaribishe wote siku ya Novemba 27 tuonekazi za wabunifu wetu wa Tanzania." amesema Augustar


Ameongeza kuwa jukwaa la Start Tailoring Business, (STB) tunategemea kuibua vipaji vya wanamitindo ambao watatumika kuonyesha mavazi yaliyo buniwa na wabunifu hao waliopata mafunzo na kushona wenyewe.


"Nipende kuwaomba watu wajitokeze kwa wingi waweze kuwashuhudia wabunifu wetu wa ndani wakifanya ubunifu wao wa mavazi mbalimbali na kutambua Sanaa yao ndio ajira yao" amesema Augustar.

0/Post a Comment/Comments