Na Richard Mrusha
Wito umetolewa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN kulikumbuka kundi la watu wenye mahitaji maalumu kama vile walemavu wa macho, kwani ni kundi linalohitaji mahitaji maalumu sana na lina uwezo wa kuongoza na kushika nyadhifa mbalimbali za madaraka na uongozi.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Evarasting legal and foundation (ELAF) inaojishughulisha na huduma za msaada wa kisheria ndugu HAMISI MASUD kwa ushirikiano na chama cha wasioona Mkoa wa Dar es salaam, wakati wa zoezi la utoaji wa Elimu ya sheria zinazowahusu watu wenye mahitaji maalumu, kwa mujibu wa sheria za jamhuri wa muungano wa Tanzania na katiba yake ambayo imezingatia haki ya usawa.
MASUD amesema kuwa walemavu wa Macho ni kundi la watu ambao baadhi yao ni wasomi na wanaelimu mbalimbali na wenye uwezo wa kuongoza na kuweza kushika nafasi mbalimbali hapa nchini na hata nje ya nchi, Taasisi hiyo kwa ushirikiano wa chama hicho wangefurahi sana kuona miongoni mwa teuzi za Rais kungekuwepo na na watu wasio na uwezo wa kuona wakiteuliwa kushika baadhi ya nyadhifa na ngazi mbalimbali.
MASUD ameishauri serikali, jamii na wadau mbalimbali kuzingatia haki za msingi zinawafikia kundi hilo la walemavu wa Macho, haswa katika swala la Elimu hususani kwa watoto wenye ulemavu wa macho, kwa kuandaa miongozo na mpango mkakati wa namna gani wanaweza wakashirikiana na wadau wa sekta ya elimu kuweza kulisaidia kundi hilo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona Mkoa wa Dar es salaam Khalid Sadick ameishukuru Serikali kwa mambo mbalimbali wanayoyafanya kwa walemavu wa macho zikiwemo teuzi chache kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa macho.n
Pia ameikumbusha Serikali kuwa bado kuna wasio ona wengi ambao wenye elimu katika ngazi mbalimbali,hivyo bado kuna uhitaji mkubwa wa kuteuliwa ama kuchaguliwa katika nafasi mbalimbali katika kuwakilisha kundi hilo.
Zoezi hilo liliambatana na matembezi yenye lengo la kuijulisha jamii na Serikali kuwatambua watu wasioona kuwa wapo katika jamii wanamahitaji mengi na pia kupata mafunzo mbalimbali ya kisheria kwa kuwa jamii ya walemavu zinazowahusu lakini wengi wao hawazijui.
Post a Comment