WASICHANA watakiwa kuzikimbilia fursa za kibiashara hasa urembo na Manukato kutokana na kupatikana na wateja wengi.
Mjasiriamali wa Manukato Penina Nguma ambae anajishughulisha na biashara hiyo kwa zaidi ya Miaka 14 amesema wakati Mwengine wasichana wamekua tegemezi na kutozikimbilia baadhi ya fursa kwa wepesi,na hivyo inatakiwa Kuanza wao wenyewe kukubaliana na Hali halisi ya Maisha na kumuunga Mkono Rais wetu Mama Samia kuchapa kazi kutokana na sera yake "Kazi iendelee".
"Nina miaka mingi nilianza na Manukato 10 lakini nilihakikisha napata Wateja kutoka sehemu mbalimbali pamoja na kuwajengea uaminifu Wateja wangu ikiwemo kuwauzia vitu vyenye ubora na kwa bei nafuu".
Aidha amefafanua kuwa baadhi ya wapenzi wa Manukato hawana Elimu ya kutosha kujua jinsi ya utumiaji wa aina za Manukato kwa miili yao hivyo kupitia duka lake la "My obsession" yupo tayari kutoa Elimu hiyo ili wateja waweze kupata vitu vizuri na sahihi kwa miili yao na ngozi zao.
Hata hivyo ameeleza kwa namna gani Miaka miwili ya Mbunifu Irfan imeweza kumjengea uwezo wa kujitokeza na kujumuika na wajasiriamali wengine tofauti tofauti kwa ajili ya kujifunza vingi sanjari na kupata Wateja wengine.
Penina ameongeza kuwa wasichana waache kuona Maisha ni mepesi kwa kujiingizia kwenye vitendo viovu kwa ajili ya kujipatia pesa za kujikimu badala yake waweze kuzikimbilia fursa.
Post a Comment