Msanii Athuman Njaidi, 'Patrick Kanumba' na Gavin Kakorosa, 'King' maarufu katika tamthilia ya jua kali, na Huba wamechaguliwa katika kuhamasisha afya ya uzazi kupitia Youngand Alive Initiative kusaidia kutoa elinu kwa watoto 14 hadi 24 na vijana.
Akizungumza na waandishi wa habari, leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi
wa taasisi ya Young and Alive Initiative, Sesilia Shirima, amesema taasisi yetu ni ya vijana yenye madhumuni ya kuimarisha afya ya uzazi
kwa vijana, hasa tukilenga kuanzia umri wa miaka 15 hadi 24 wa vijana bahele.
"Taasisi yetu ilianza 2017 na wenzangu wachache tukiwa
masomoni, tulikuwa tukifanya masomo ya utabibu katika chuo cha
maafisa tabibu mkoa wa Mtwara."
Aidha aliongeza kuwa Patrick Kanumba na King in moja ya wadau ambao ni vijana watakao saidia kuamashisha vijana wenzao.
"Klabu ya afya ya uzazi ya maafisa tabibu, tuliweza kutembelea vijana
wengi Mtwara kuanzia mashuleni na kwenye jamii, tuliwafundisha namna
ya kujikinga na mimba, na maambukizi ya magonjwa ya ngono."
"Tulipo maliza masomo, tuliona haitoshi ni vyema tukaendeleza juhudi zile
huku mtaani, tukaamua kuanzisha taasisi tuliyooita young and alive
initiative, shughuli zetu nyingi zilijikita nyanda za juu kusini, mkoa wa
mbeya, songwe na njombe tukishirikiana kwa ukaribu sana na serikali za
mikoa na wilaya na kamati za afya katika kuwajengea uwezo vijana
kutambua haki zao za msingi za afya ya uzazi ikiwemo haki ya kupatiwa
taarifa sahihi za afya ya uzazi, na huduma rafiki za afya ya uzazi.
Taasisi yetu hamu yake kubwa ni kuona Tanzania yenye vijana wenye afya
na wanao tambua haki zao za afya ya uzazi, wanaweza kujikinga kutopata
mimba na kujikinga na maambukizi ya magonjwa ya ngono ikiwemo
maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Sasa leo tumekuja mbele yenu tukiwatambulisha programu yetu ya YAI
fellowship, kama tulivyo wajuza taasisi yetu inaitwa young and alive lakini
haimaanishi sisi tutakuwa young milele, na tukizeeka haimaanishi jitihada
za vijana kama hizi pia ziishe, kwa hivyo lengo la mradi wetu ni kujenga
uwezo kwa vijana kuanzia miaka 15 mpaka 24 kutambua na kuwa
viongozi katika kufikisha taarifa za afya ya uzazi kwa vijana wenzao na
huduma kwa kutumia nguzo tatu za uongozi kama utoaji huduma,
uchechemuzi na ujasiriamali jamii.
programu ya YAI fellowship, yaani mafunzo haya ya uongozi katika nguzo
hizi tatu, hayatakuwa ya mara moja tu, yatakuwa yamgawanyiko wa mara
kwa mara, kwa muda wa miezi nane.Tutakuwa tukishirikiana na wadau
mbalimbali kufanya mafunzo haya, mfano tutahusisha wadau wanaofanya
uchechemuzi, ujasiriamali jamii na utoaji huduma ili waweze kutoa ujuzi
wao kwa vijana hawa.
Serikali yetu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imesisitiza sana kwetu
sisi mashirika yasiyo ya kiserikali kufanyia kazi vipaumbele vinavyo
endana na vipaumbele vya nchi, hivyo basi program yetu ni sehemu ya
vipaumbele vya serikali.
Mfano mwaka huu kwa mara ya kwanza serikali
imetoa mpango wa kuimarisha afya kwa makundi ya vijana balehe,
mpango ambao ume ainisha mikakati madhubuti ya kuimarisha afya ya
kundi hili la vijana.
Katika mpango huu vipaumbele vitatu vikubwa
vilivyowekwa inajumuisha kupunguza maambukizi ya virusi ya UKIMWI
kwa vijana, kupunguza mimba za utotoni na kupunguza ukatili wa kijinsia.
Ukiangalia vipaumbele hivi vitatu vikubwa vyote vinalenga eneo la afya ya
uzazi na hivyo jitihada za kuhakikisha mpango huu unatimia zinatuhitaji
sisi vijana.Ukiachilia mpango huu bado kuna sera zingine kama vile
mpango wa kumaliza ukatili wa kijinsia na sera ya vijana ya taifa.
Post a Comment