TAULO ZA KIKE ZA KUFUA ZAKADIRIWA KUPUNGUZA MATATIZO YA MFUMO WA UZAZI KWA WANAWAKE


Mjasiriamali pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Jollie Mwanaidi Mwilima, Kampuni inayojishughulisha na utengezaji wa vifaa tiba (Taulo za kike za kufua)

Miongoni mwa vifaa tiba (Taulo za kike)ambazo hazina kemikali yoyote ni salama Kwa matumizi zilizotengenezwa na Mwanaidi Mwilima kutoka Kampuni ya Jollie
..........................
    
  Na.Khadija Seif, Michuzi TV

WADAU wa Afya waombwa kuongeza nguvu hususani vijijini kutoa elimu ya Hedhi salama kwa Mabinti Ili kupunguza matatizo katika Mfumo wa uzazi kutokana na matumizi ya vifaa tiba visivyo salama na hatarishi.

Akizungumza na Michuzi Mkurugenzi wa Kampuni ya Jollie Mwanaidi Mwilima ,ambae ni Mtengenezaji wa Taulo za kike za kufua pamoja na nepi za kufua amesema elimu ya jinsi ya kukabiliana na hedhi salama bado ni kipengele kizito kutokana na wazazi au walezi kutojipa muda wakuzungumza na watoto wao pamoja na Hali ya uchumi kuwa changamoto kwao na kutoweza kumudu gharama za kujiweka salama.

"Mabinti wamevishwa taswira ya kutumia vitu hatarishi ambavyo badae vinaleta madhara katika mfumo wa uzazi ikiwemo vitambaa ambavyo sio salama,majani ya mgomba Kwa walio vijijini na Nyenzo nyingine nyingi Kwa ajili ya kujikingia hivyo wazazi wanatakiwa kuzungumza na mabinti Ili tuone Kwa namna gani tunampa furaha Binti awepo kwenye siku zake na kuhakikisha anapata hedhi salama."

Hata hivyo Mwilima ameeleza Kwa namna gani alipata msukumo wa kutengeneza Taulo hizo za kike za kufua zenye matumizi endelevu na zisizoleta madhara ya aina yoyote Ile na kumhakikishia usalama mtumiaji zisizokua na kemikali yoyote ile.

"Wakati Niko kwenye harakati za kufanya uchunguzi Kwa namna gani tutaweza kuwapa furaha mabinti katika siku zao nilikutana na Binti ambae alipata madhara baada ya kutumia Taulo za kisasa pamoja na mwengine kutumia njia ambayo si Salama Kwa Afya ya uzazi nikawiwa kutengeneza taulo hizo ambazo ni nzuri na salama Kwa matumizi."

Pia ameongeza kuwa wazazi,wadau wa Afya,Mashirika na walimu wasisite kuzungumza na mabinti kuhusu hedhi salama Ili kuwajengea uwezo wa kufanya vizuri darasani. 

0/Post a Comment/Comments