UN VOLUNTIA WATOA MAFUNZO YA KUJITOLEA KWA WANAFUNZI SUZASO


 Mkufunzi wa Mafunzo ya fursa za kujitolea Penina Nguma akisikiliza kwa makini Mawasilisho ya viongozi wanufaika wa Mafunzo yaliyotolewa na Umoja wa Mataifa UN hapa nchini kuhusu vijana kuzikimbilia fursa mbalimbali zinazotolewa na Makampuni,Taasisi Jumuiya ,Mashirika kwa lengo la kukuza Maendeleo ya Taifa.


Picha ya pamoja baina ya Mkufunzi wa Mafunzo ya fursa mbalimbali za kujitolea kutoka Umoja wa Mataifa (UN) Penina Nguma pamoja na wanufaika wa Mafunzo hayo viongozi wa Chuo Kikuu Zanzibar (SUZASO).


*******************************************

   Na.Khadija Seif, Michuzi Tv

VIJANA nchini wameaswa kujitokeza kutengeneza fursa mbalimbali za kibiashara hususani fursa za kujitolea kukuza Maendeleo ya Taifa.


  Akizungumza na Michuzi Tv,Mara baada ya kutoa Mafunzo hayo Mkufunzi kutoka Umoja wa Mataifa (UN) Voluntia Penina Nguma amesema Ni vizuri Vijana hususani wanafunzi Katika vyuo Vikuu  kujijengea uwezo wa kujikita kujitokeza kwenye fursa mbalimbali zinazotolewa na Makampuni,Taasisi,Jumuiya,Mashirika au watu binafsi kwani zinawajengea uwezo wa kutafuta ajira, kutafuta Masoko kutokana na mikusanyiko au watu wanaokutana nao katika fursa hizo za kujitolea. 


"Wasitazame nafasi walizonazo au hata vyeo vyao lakini wajitolee kwa lengo la kuimarisha na kuboresha Maendeleo yetu nchini kwa Mustakabali wa Taifa kwa ujumla bila Kujali maslahi." 


Hata hivyo Nguma ameongeza kuwa wanafunzi Katika vyuo Vikuu waweze kukimbilia fursa za kujitolea hata kama hakuna faida za awali wanazopata ila kadri wanavyoweza kujitangaza na kufanya kazi Kwa bidii wataweza kunufaika na kuyaona Matunda kwa siku za baadae.  


 Nae Rais wa Chuo Kikuu Cha Zanzibar  (SUZASO) Sleyum Abdallah  amepongeza uongozi wa Umoja wa Mataifa UN kwa kutoa Mafunzo kwa wanafunzi wa chuo hicho.  


"Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wanafunzi wa vyuo vikuu katika Majukumu yao".


Abdallah amefafanua faida walizopata katika Mafunzo hayo ikiwemo kufuta taswira iliyojengeka hapo awali kuwa katika fursa za kujitolea hakuna faida yoyote badala yake fursa hizo zinalenga kumjengea umakini pamoja na kukuza mtandao kwa watu mbalimbali.


Nae Mmoja ya viongozi wanufaika wa Mafunzo hayo yaliyotolewa kwa siku 1 katika Chuo kikuu Cha Zanzibar kwa viongozi 24, Salum Ally amesema kupitia Mafunzo hayo Vijana wengi wataweza kujijengea uaminifu,uadilifu na Moyo wa kujitolea katika kazi zozote zile.

0/Post a Comment/Comments