WAHITIMU 1,517 KUTOKA UDSM WATAKIWA KUITUMIA VYEMA ELIMU WALIYOIPATA CHUONI.


Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM),Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Kikwete akiwatunuku Digrii mbalimbali wahitimu waliohitimu Stashahada na Astashahada  katika Chuo hicho katika mahafali yaliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Mlimani City.

Baadahi ya wahitimu ambao wamehitimu na kutunukiwa Shahada za awali na waliohitimu Stashahada na Astashahada  katika Chuo Kikuu Cha Dar es salaam  (UDSM)

.....................................

NA MUSSA KHALID,DAR ES SALAAM

Jumla ya Wanafunzi wapatao 1,517 ambao wamehitimu na kutunukiwa Shahada za awali na 48 waliohitimu Stashahada na Astashahada  katika Chuo Kikuu Cha Dar es salaam  (UDSM) wametakiwa kwenda kuitumia elimu waliyoipata kama ushawishi kwa watu wote lakini pia wajihadhari na UVIKO-19 

Hayo yamejiri leo jijini Dar es salaam katika Duru ya nne ya  Mahafali ya 51 ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) ambapo mgeni Rasmi na Mkuu wa Chuo hicho,Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Kikwete amewatunuku Digrii mbalimbali wahitimu hao .

Akizungumza katika Mahafali hayo,Mkuu wa Chuo UDSM Dkt Kikwete ametumia fursa hiyo kuwataka Wahitimu hao kuendelea kuchukua tahadhari ya UVIKO 19 sambamba na kuepuka kusikiliza maneno yasiyokuwa ya wataalamu wa Afya.

Awali akizungumza Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof.William Anangisye amesema Chuo hicho kinajivunia mafanikio makubwa hasa kwa kuongeza fedha za Utafiti kutoka shilingi milioni 712.8 mwaka 2018 wakati utaratibu huu unaanza hadi kufikia zaidi shilingi bilioni tatu mwaka 2021/2022. 

"Katika kuboresha na kuongeza ufanisi, mwaka huu Chuo Kikuu kimeamua kuwa kati ya fedha hizo ni kwa ajili ya uvumbuzi (Innovation) fedha ambazo zinatokana na vyanzo vya ndani vya fedha". Amesema Prof.Anangisye

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jaji Mstaafu Damiani Lubuva amesema Baraza limeendelea kutoa ushauri na maelekezo mbalimbali kwa Chuo ili kuhakikisha kuwa lengo la utoaji elimu, utafiti na ushauri wa kitaalamu linafanikiwa . 

"Baraza linaendelea na juhudi mbalimbali za kuzishughulikia changamoto hizo kwa kutumia fedha inazopata Serikalini na pia kwa kutumia vyanzo vyake vya ndani". Amesema Mhe.Lubuva.

Kwa upande wao baadhi wahitimu wa chuo hicho,wamesema watakwenda kuielimisha jamii katika mfumo ambao utawasaidia watanzania katika Nyanja mbalimbali.

Hata hivyo wahitimu hao wamekumbushwa kujiunga na jamii kama nguvu kazi muhimu hivyo ni vyema wakawa wepesi kujifunza mambo mapya.

0/Post a Comment/Comments