ZIC YAFANYA MAZUNGUMZO NA AMGL



MKURUGENZI wa Shirika la bima Zanzibar (ZIC) Arafat Haji amekutana na Mkurugenzi wa Africa Media group limited (AMGL) Shaban Kisu na kufanya Mazungumzo.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi za AMGL na wakurugenzi wamekubaliana Ushirikiano wa karibu katika Kampuni zao kwa ajili ya kuleta Maendeleo katika Taasisi wanazoziongoza.

Hata hivyo Shirika la Bima (ZIC) ni Miongoni mwa Shirika ambalo limepongezwa siku za karibuni kwa uchapakazi wake  na kuhakikisha wananchi wanapata bima kwa Bei nafuu na kufanya malipo yao (Kiganjani) Kwa njia ya  mtandao wa vodacom.

Huduma za bima zinazopatikani katika Shirika Hilo ni bima ya nyumba na Makazi,bima ya ajali,bima ya Afya kwa ujumla pamoja na zingine nyingi.
 

0/Post a Comment/Comments