BUNGE LAUKATAA UCHAGUZI WA RAIS LIBYA

 


Kamati ya bunge la Libya imesema leo kuwa haitawezekana kuandaa uchaguzi wa rais uliosubiriwa kwa muda mrefu katika siku mbili zijazo kama ilivyopangwa. ‘


Hilo ni pigo kubwa kwa juhudi za kimataifa za kuumaliza muongo mmoja wa machafuko katika nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta. 


Hiyo ni taarifa ya kwanza rasmi kuwa uchaguzi huo hautofanyika Ijumaa, ijapokuwa hilo lilitarajiwa kutokea kutokana na kuongezeka kwa changamoto nyingi na wito wa kutaka uahirishwe.


Katika barua yake kwa spika wa bunge Aguila Saleh, mbunge al-Hadi al-Sagheir, mkuu wa kamati hiyo ya bunge iliyopewa jukumu la kuufuatilia mchakato wa uchaguzi, amesema wamegundua kuwa uchaguzi huo hauwezi kuandaliwa Desemba 24.


Hakufafanua kama tarehe nyingine imepangwa, au kama uchaguzi huo umefutwa kabisa. Tume ya uchaguzi ilizivunja kamati za uchaguzi jana jioni, na haikutaja orodha ya mwisho ya wagombea kama ilivyohitajika kufanya.


0/Post a Comment/Comments