DC MASALLAH AZINDUA TAWI LA EFM JOGGING CLUB MWANZA





         ******************************

Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mkoa wa Mwanza Mheshimiwa Hassan Masallah leo amezindua tawi la EFM Jogging Club Mwanza.


Uzinduzi  huo umefanyika katika Ukumbi wa Al Muzamil Hotel ambayo iko Mtaa wa Uhuru Mwanza Mkabala na Hospitali ya Uhuru.


Sabamba na uzinduzi wa tawi hili, pia DC Masallah amezindua  jezi rasmi ya mazoezi ambayo itakuwa inatumika katika mbio mbalimbali zitakafanyika Mwanza na nje ya mkoa wa Mwanza.


Akimkaribisha DC Masalla, Mwenyekiti wa EFM Jogging Makao Makuu Ramadhani Msoza Bin Rashid amesema wamemwalika Mkuu wa Wilaya maana ni mtu wa Mazoezi.


"Tunamshukuru DC Masalla kwa kuja, ni kweli tulikuwa na wageni wa kuwaalika ila tumeona tumkaribishe yeye aje atuzindulie tawi na jezi zetu"


DC Masalla amewaasa watu wote katika Mkoa wa Mwanza hususani Wilaya za Ilemela na Nyamagana kujijengea tabia ya kupenda mazoezi Ili kujinusuru na magongwa nyemelezi.


"Mazoezi ni Afya, Mazoezi ni Mtaji, ninawaomba wananchi wote wa Mkoa wa Mwanza, kushiriki katika Mazoezi ya viungo Ili kujilinda na magongwa mbalimbali" 


Vilevile DC Masalla amewaomba wananchi wote kesho Jumamosi kushiriki katika mbio za kilomita nane za  Ilemela Jogging zitakazoanzia Uwanja wa  Sabababa Ilemela Saa 12 Alfajiri.


Uzinduzi wa EFm Jogging Club inaongeza idadi ya klabu za Jogging mkoani Mwanza ambayo Makao Makuu yake yatakuwa Kata ya Kirumba Wilaya ya Ilemela Mkoa wa Mwanza na tayari imeanza kusajili wanachama wapya Ili kujiunga na EFM Jogging Club Mwanza.

0/Post a Comment/Comments