Meneja Masoko wa Kampuni ya Alaf Saluwa Aziz akiwa sambamba na Maulid Kitenge akiwa kama balozi wa Huduma ya Mfumo wa kidigitali wa kufanya Manunuzi ya vifaa vya ujenzi kupitia kiganjani.
**************************************
Na.Khadija Seif, Michuzi TV
KAMPUNI inayotengeneza Mabati aina ya Alaf imewasogezea Huduma karibu wateja wake Kwa Mfumo wa kidigitali zaidi Ili kurahisisha Huduma zao za vifaa vya ujenzi.
Akizungumza na waandishi Wahabari wakati wa kutambulisha Huduma hiyo mpya Kwa kununua vifaa vya ujenzi wa mbalimbali ikiwemo Mabati na kuundwa program ambayo itawezesha Manunuzi na uchaguzi wa vifaa kiuweledi.
"Mfumo huo itamuwezesha mteja kuchagua Vifaa mbalimbali na kufanya malipo Kwa njia ya Mtandao ,Meneja Masoko Saluwa Aziz amesema kutokana na kuwepo Kwa Mabadiliko ya Hali iliyopo Kwa Sasa na Taifa kupata janga la ugonjwa wa uviko hivyo Kampuni yao imejali Huduma zao na kuziboresha zaidi hivyo Kwa Sasa wateja wataepuka misongamano hasa Madukani na kufanya Manunuzi Kwa Mfumo kidigitali."
Hata hivyo Saluwa ameongeza kuwa kuzinduliwa Kwa Mfumo huo itasaidia pia kuwawezesha hata waliopo mbali na maeneo husika ya ujenzi hususani waliopo nje ya Mkoa au Nchi kurahisisha ununuzi wa vifaa hivyo kusaidia ujenzi kuendelea.
Pia Meneja Masoko amewahakikishia wateja kuboresha zaidi Huduma zao na kuleta vitu vizuri ikijumuisha utafiti ambao Kampuni hiyo imekua ikifanya Kwa ajili ya kuleta bidhaa nzuri sokoni.
Mmoja ya Mteja ambae amepata Huduma za vifaa vya ujenzi kupitia programu hiyo Janeth John amesema ni Huduma ambayo inamuhakikishia uaminifu mteja kwani anachagua kitu ambacho anaiona ubora wake na kuchagua Kwa kiwango gani angetaka kifaa hiko kuanzia Michoro,ukubwa pamoja na Bei halisi.
Post a Comment