Waziri wa Mambo Ya Ndani George Simbachawene ameongoza zoezi la kuteketeza silaha 5230 ambazo zimekusanywa kwa kipindi cha mwaka 2018 hadi October 2021ambazo zimepatika kwenye matukio mbalimbali ya kiuhalifu.
Akizungumza leo katika zoezi la uteketezaji wa silaha hizo a katika viwanja vya Shabaha jijini Dar-es-salaaam, amesema serikali itaendele kutoa ada za michango ya mwaka ili kuiwezesha sekretalieti kufanya majukumu yake kikamilifu.
"Tukiwa tunafunga maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia nikumbushe tuu silaha zimekuwa zikitumika katika kutekeleza ukatili wa kinjinsia hivyo tunapaswa kuzifichua ili kukomesha ukatili huu ,serikali ya Tanzania itahakikisha kuww inasimamia hali ya usalama wa nchi na watu wake". amsema waziri simbachawene.
Waziri amesema analipongeza jeshi la polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kwa kufanikiwa kukamata silaha ambazo zilikuwa katika mikono ya wahalifu.
Nae Mkuu wa jeshi la Polisi Simon sirro amesema takwimu za silaha ambazo zinateketezwa leo kwa kipindi cha mwaka 2018 mapaka oktoba 2021 ni Magobole 3724, Rifle 573, pisto 20, G3 1, AK47 111, ASR 5 , shourtgun 789, FA 7.
Kwa upande wa Kamshina Msaidizi wa Polisi na Mkuu wa kitengo cha uthibiti wa silaha Renada Milanzi amesema kauli mbiu na la zoezi hili ni Fichua silaha haramu kwa maendeleo endelevu ya Nchi.
"Silaha 5230 zimepatika kwenye matukio mbalimbali katika operation ya kuondoa silaha haramu katika nchi yetu, kesi mbalimbali amabzo mahakamani zimetoa uhamuzi wa kutahifisha silaha kutoka kwa wamiliki ambao wamekeuka sheria ya umiliki wa silaha ya 2015"Amesema Renada
Aidha amesema tukio hili litafanyika kwa Makubaliano mbalimbali ya kimataifa na Makubaliano ya umoja wa Afrika.
Kwa upande Mkuu wa mkoa Amos makala amesema zoezi hili litawajenga wananchi uelewa kuhusiana na silaha haramu na kuwaomba wananchi kutoa taarifa kw jeshi la polisi pale pale wanapo baini mtu ambae anatumia silaha kinyume cha sheria.
Post a Comment