................
Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
TAMASHA La Waokaji lalenga kupanua biashara ya keki na kuwakutanisha wapishi pamoja na wateja wengine wapya Ili kuwajengea motisha ya kujiajiri.
Akizungumza na Michuzi Muandaaji wa Tamasha la Waokaji Jijini Dar es salaam Manka Rajab amesema Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika disemba 12 mwaka huu katika ukumbi wa Hekima uliopo Mikocheni jijini Dar es salaam na kutarajiwa kuhududhuriwa na watu mbalimbali ikiwemo Waokaji kutoka Mikoa tofauti tofauti.
Manka ameeleza lengo la kuandaa Tamasha hilo ni kupanua biashara ya keki na kuwakutanisha Waokaji kutoka sehemu mbalimbali Ili kupeana ma kubadilishana ujuzi
"Kwa mara ya kwanza tunafanya Tamasha letu na litafanyika katika ukumbi wa Hekima uliopo Mikocheni tunategemea tutapeana na kujuzana mengi katika Tamasha letu ikiwemo kupika keki mubashara na kutayarisha vifaa vya uokaji vitafunwa na keki kwa wapishi ambao tayari wamejisajiri kushiriki Tamasha letu".
Hata hivyo Manka ameeleza zaidi lengo la kuandaa Tamasha la Waokaji Kwa mara ya kwanza .
" Tamasha letu linalenga kuwakutanisha Waokaji sehemu mbalimbali Ili kupeana maarifa zaidi ya kuboresha biashara hiyo,namna ya kutafuta wateja na kubadilishana ujuzi".
Pia ameongeza kuwa muitikio mzuri na tayari maandalizi ya Tamasha hilo linaendelea vizuri na takribani washiriki 60 wameshachukua fomu za ushiriki .
Post a Comment