Muongozaji wa Filamu ya "Binti " Seko Shamte akizungumza na waandishi Wahabari pamoja na wadau wa Filamu kuwahabarisha kwa Sasa Filamu yake ya "Binti" inapatikana katika Mtandao wa Kimataifa wa kuonyesha Filamu Netflix
************************************
Na.Khadija Seif, Michuzi TV
FILAMU ya Binti yazidi kuipeperusha bendera ya Tanzania duniani kwa kuingia kwenye Mtandao wa kupakua Filamu wa Dunia Netflix.
Akizungumza wakati wa kutambulisha filamu hiyo ya Binti Mtendaji Mkuu wa Bodi ya filamu nchini Kianzo Kiagho amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaendelea kutoa ushirikiano mzuri Kwa wadau wa tasnia ya filamu na Kwa mwaka 2021 kumefanyika Tuzo za filamu Kwa mara ya kwanza zenye lengo la kutambua Mchango wa Sanaa ya filamu nchini.
" Miongoni mwa walioshiriki katika filamu ya Binti ndio Moja ya zao la Tuzo za filamu na ambae ndio Msanii wakike 2021 hivyo utaona alistahili na hakukua na janja janja ya aina yoyote Ile kupitia mchakato mzima uliofanyika wakati wote."
Hata Kiagho ameeleza kuwa Kwa mwaka huu Serikali imeweza kutenga Fedha Kwa ajili ya kuboresha upande wa utayarishaji wa kazi za Sanaa ambao watayarishaji watakopeshwa bila riba Ili waweze kutengeneza kazi zao Kwa weledi unaotakikana pamoja ubora wa Hali ya juu.
"Mtandao wa Netflix unahitaji kazi zenye ubora zaidi na kilio Cha baadhi ya watayarishaji ni swala la Fedha hivyo Serikali imetenga Fedha Kwa mwaka watapatiwa utaratibu jinsi ya kuweza kupata Fedha hizo na tunategemea tutapeleka filamu nyingi Netflix na Kwa namna Moja au nyingine tutatangaza Rasilimali tulizonazo nchini kwetu."
Hata hivyo Kwa upande wake Muongozaji Mahiri Seko Shamte amesema filamu ya Binti imeweza kukidhi vigezo vya kuingia Netflix ambapo uzinduzi wake ulifanyika mwaka 2021.
" Ni filamu yangu nyingine ambapo nimeshatengeneza filamu ya "Home coming",Makala ya Mkwawa pamoja Filamu ya binti ambayo imefanikiwa rasmi kuingia Netflix na imeshapata Tuzo za ziff ."
Aidha ,Seko amefafanua sababu ya Filamu za bongo kutoingia kwenye Mtandao wa Netflix na kupelekea kuonekana hakuna nafasi ya kuwepo Kwa kazi zao .
"Hatuna wasambazaji wa kutoka Tanzania ambao wanapeleka kazi zetu huko japo nilipata nafasi baada ya Media ya Okada kutoka Kenya kusaini Mkataba wa kuwa wakala wa kazi zetu."
Hata hivyo Mmoja ya washiriki katika Filamu hiyo ya "Binti" ambae aliweza kusinda Tuzo ya Msanii Bora wakike Kwa mwaka 2021 katika Tuzo za Filamu nchini kupitia bodi ya Filamu ikishirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Godliver Gordian ametoa pongezi Kwa wadau wa tasnia ya filamu Kwa kuendelea kuonyesha jitihada nyingi kuwezesha Wasanii wakitanzania wanafikia Masoko ya ndani na nje ya nchi.
"Bodi ya filamu ni Miongoni mwa muhimili mkuu ambao umetuunga Mkono Kwa kiasi kikubwa pamoja na Kuonyesha juhudi na kuendeleza Sekta hii ya filamu nchini Kwa namna Moja au nyingine".
Gordian ameeleza Kwa namna Mtandao wa Netflix utaweza kuwanufaisha watanzania hususani Wasanii wa Bongomovie pamoja na kutangaza utalii uliopo nchini na kuwasihi watayarishaji wa filamu ipo haja ya kuongeza ubunifu katika kazi za Sanaa kwani Kwa Sasa Mtandao huo utawapa uwanja Mpana sana kujitangaza.
Binti ni filamu ambayo inaelezea Maisha ya Mama wakiafrika ambae sio tegemezi ana pambana Kwa ajili ya Maisha ya watoto wake na familia Kwa ujumla.
Post a Comment