Kampuni ya Kitanzania Afrieuro Digital Ventures yenye leseni ya kuuza na kuendesha majukwaa ya matangazo/mifumo ya Kupatana.com na Zoomtanzania.comi imesema itaendelea kuongeza wigo wake kwa upana zaidi katika kukuza soko la uhakika mtandaoni nchini Tanzania
Imeelezwa kuwa Mwishoni mwa mwaka jana Afrieuro Digital Ventures ilifanikiwa kupata haki za kipekee za kuuza na kuendesha tovuti hizo mbili zilizoainishwa ambazo zote zinatumika kwa upana nchini Tanzania
Majukwaa hayo mawili, Kupatana.com na Zoomtanzania.com, yamekuwa washindani wa muda mrefu lakini sasa yataunganisha nguvu ili kutoa huduma zake kwa urahisi, haraka na salama zaidi kwa wanunuzi na wauzaji mtandaoni.
Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Afrieuro Digital Ventures " Makusaro Tesha, amesema hiyo ni fursa nzuri haswa kwa watumiaji wa mitandao walio Tanzania kwa kuwa wataweza kukuza na kuboresha zaidi uwepo wa uhakika wa soko la mtandaoni na kutoa fursa zaidi za mauzo na matumizi rahisi ya mifumo hiyo kwa watumiaji wa ina zote.
Amesema mpango uliiopo kwa mwaka huu ni kuzindua tovuti mpya ambayoitaiunganisha mifumo hiyo miwil ambayo itakuwa ni toleo jipya litakalojumuisha mifumo hiyo miwili, lakini pia itakuwa na vipengele vipya ambavyo vitawawezesha watumiaji wa mitandano kuendelea kufurahia upatikanaji wa huduma mitandaoni kwa usalama
‘Kwa mtazamo wa kiufundi, tovuti hiyo mpya itakuwa ni toleo jipya litakalojumuisha mifumo hiyo miwili, lakini pia itakuwa na vipengele vipya ambavyo vitawawezesha watumiaji wa mitandano kuendelea kufurahia upatikanaji wa huduma mitandaoni kwa usalama, haraka na njia kirafiki zaidi ya kununua na kuuza bidhaa na huduma mitandaoni’anasema Makusaro Tesha.
Post a Comment