Mwenyekiti wa Chama cha siasa cha NCCR
Mageuzi James Mbatia amesema Job Ndugai bado ni Spika wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa mujibu wa Katiba ya nchi.
Mbatia ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es
salaam wakati akizungumza na wanahabari ikiwa ni siku moja baada ya Spika wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai kuandika barua ya kujiuzulu kwa
Katibu Mkuu wa CCM akisema kuwa alipaswa kuandika barua hiyo kwenda kwa Katibu
wa Bunge.
Mwenyekiti huyo amesema mambo yote
yanayoendelea kwa sasa nchini bado ni Afya kwa taifa kutokana na watanzania
wanaendelea kuyajadili hoja ya usalama wa Taifa hivyo ni vyema yasichukuliwe
hasi ili taifa lisiweze kuparanganyika.
Aidha amesema utaratibu wa Namna Spika
kujiuzulu uko kwenye katika ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya
149(1)(c) kuwa iwapo mtu huyo ni spika au Naibu Spika wa Bunge basi taarifa
hiyo ya kujiuzulu iwasilishwe kwenye Bunge hivyo ameeleza migongano inayoendelea
ni vyema ikasimamiwa ili taifa liwe kwenye usalama.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo amewashauri viongozi na wadau mbalimbali wakiwemo wastaafua kuandaa meza ya mazungumzo ili kujadili yanayoendelea nchini.
Post a Comment