Ewura imetangaza ukomo wa bei mpya ya mafuta nchini huku mafuta ya Petroli ikishuka hadi tsh. 2994 kwa Lita.
Taarifa iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari inaonyesha kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia bei mpya ilipaswa kuwa tsh. 3310 kwa Petroli na tsh. 3452 kwa Dizeli.
Lakini kutokana na ruzuku iliyoingizwa na serikali ya bilioni 100 kwenye mafuta sasa bei mpya ya bidhaa hiyo imeshuka hadi kiasi cha shilingi 2994 kwa Petroli na shilingi 3231 kwa mafuta ya Dizeli.
Bei hizi zinaanza kutumika tarehe Mosi June, 2022 nchini nzima.
Post a Comment