MWENYEKITI MTEMVU AMEWATAKA WANA CCM KUJENGA UMOJA



 ......................

Na Heri Shaaban (CCM)

MWENYEKITI wa chama cha Mapinduzi (CCM) Abas Mtemvu amewataka Wana CCM mkoa Dar es Salaam kujenga Umoja na Mshikamano kuakikisha Wana safiri pamoja kutetea chama cha Mapinduzi kiweze kushika Dola katika chaguzi zake zote .

Mwenyekiti Abas Mtemvu ,amesema hayo Dar es Salaam Ofisi ya CCM mkoa wakati wa mapokezi yake alipokaribishwa rasmi .

"Nawaomba wana ccm wangu wa mkoa huu tujenge umoja na Mshikamano tusafiri pamoja kila wakati katika kukitetea chama chetu " alisema Mtemvu .

Mwenyekiti Abas Mtemvu, alisema alijua mechi atashinda leo amekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa alipambana na wachezaji wa timu mbalimbali mwisho wa siku akachaguliwa yeye .

Aliwataka wana CCM wawaone kina Mtemvu wazuri katika Uongozi wake watasimamia haki kila sehemu pamoja na Kamati yake ya siasa .

Akizungumzia Serikali ya awamu ya nne alisema Madiwani wa Temeke walimshauri agombee Ubunge aligombea akashinda Kwa kishindo ,anamshukuru , RAIS Jakaya Mrisho Kikwete alimpa ushirikiano mkubwa wakati wa Ubunge wake Temeke na miradi ya Maendeleo zikiwemo BARABARA za kisasa za Mradi wa DMDP zimeweza kubadilisha Temeke yote na Changombe.

Akizungumzia CCM alisema katika uongozi wake watasimamia haki amna mtu atakaye onewa CCM ya mafunzo Watu wakigombana Wana weka CCM wapya ,Pia ataki kusikia Naibu Spika ambaye ni Mbunge wa Ilala anasumbuliwa badala yake washirikiane kuondoa kero Dar Salaam .

Mnec wa CCM mkoa Dar es Salaam Juma Simba Gadaf amewapongeza Viongozi kwa kurudisha jina lake na kufanikiwa kushinda kwa ushindi mnono 

Simba Gadaf alisema yeye amelelewa Dar es Salaam na Wazee yupo mikono salama kwa ajili ya kujenga chama na SERIKALI 

Aliwataka wana CCM wa Mkoa huo kuwapa ushirikiano Viongozi kwa ajili ya kujenga chama na JUMUIYA

""Sisi ni Viongozi tuokomaa atuwezi kulipiza kisasi ametaka tuwe pamoja kujenga umoja katika kumsaidia Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika utekelezaji wa Ilani ya Chama cha mapinduzi "alisema Gadaf

Mwisho

0/Post a Comment/Comments