RUWASA-MRADI WA MAJI RUDUGA MAWINDI KUNUFAISHA VIJIJI SITA MBARALI MBEYA

 

..........................

Na Mwandishi wetu Mbeya

Takribani Vijiji sita katika Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya vinatarajiwa kunufaika na huduma ya maji kutoka mradi wa Ruduga Mawindi ili kuwaondolea changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa Maji na usafi wa mazingira vijijini -RUWASA Mhandisi Clement Kivegalo katika ziara ambayo ameifanya kwenye mradi mkubwa ambao umetekelezwa na RUWASA katika Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

Mhandisi Kivegalo amesema mradi huo wamelenga kuhudumia vijiji sita na mpaka sasa tayari wameshakiwezesha kijiji cha Kangaga katika awamu ya kwanza ya mradi huo.

‘Tangu mwaka jana kwenye mwezi wa sita au wan ne wananchi wa Kangaga wamekuwa wakipata huduma ya maji safi hivyo serikali pia imefikia hatua nzuri katika kuhakikisha na vijiji vitano vilivyobakia vinapata maji’amesema Mhandisi Kivegalo

Aidha Mhandisi Kivegalo amekipongeza kijiji hicho kwa kuonyesha uwezo katika usimamizi wa maji kwani malengo yao yalikuwa ni kukusanya Mill 1 kwa mwezi lakini kwa sasa wanakusanya laki nane jambo ambalo ni mafanikio.

Pia Mhandisi Kivegalo ametumia fursa hiyo kumpongeza mkandarasi anayetekeleza mradi huo kutokana na kuonyesha jitihada katika utekelezaji wake hivyo kuleta manufaa kwa wananchi.

Awali akiyataja mafanikio ya mradi huo Msimamizi wa Chombo cha watoa huduma ya maji ngazi ya jamii Luduga mawindi Frank Sanga amesema katika kipindi cha uendeshaji wa skimu ya maji wamefanikiwa kuwafungia dira za maji wateja 220.

Amesema mafanikio mengine waliyoyapa ni ufuatiliaji wa matengenezao ya mara kwa mara katika bomba kuu huku akieleza mipango waliyonayo pia ni kuongeza vitendea kazi lakini pia kufikisha jumla ya wateja 600 wa majumbani.

Naye Mwakilishi wa wanawake Kijiji cha Kangaga Wilayani Mbarali mkoani Mbeya Flora Kweya ameishukuru serikali kwa kuwapelekea neema hiyo ya maji kwani walikumbana na adha

0/Post a Comment/Comments