******
Timothy Marko
KAMPUNI YA Azam Media wamezindua Tamthilia mbili(2) mfululizo ambazo ni MTAA WA KAZAMOYO na LORITA, Uzinduzi wa Tamthilia hizo umefanyika leo Julai 25, 2023 katika hoteli ya Hyatt (Kilimanjaro) Posta Jijini Dar es salaam.
Tamthilia hizi mbili zimebeba simulizi za kuvutia na pia zimekuja kuleta Mapinduzi ya tasnia ya tamthilia nchini kwani zinaakisi maisha halisi ya Mtanzania wa rika zote na zinahusiha waigizaji wenye vipaji na viwango vya juu.
Hakika uzalishaji wa Tamthilia hizi mbili MTAA WA KAZAMOYO na LORITA umezingatia mahitaji ya soko kwani wametumia vifaa vya uzalishaji vya kisasa na ubora wa hali ya juu wenye uwezo wa kutoa kazi katika viwango vya picha zenhe ubora na angaavu yaanj HD(High Definition), Azam media dhamira yao ni kutoa burudani ya hali ya juu kwa watazamaji wote.
MTAA WA KAZAMOYO ni tamthilia inayosimulia hadithi inayohusu maisha ya uswahilini na matukio wanayopitia wakazi wa mtaa wa kazimoyo,Huu ni mtaa wenye sifa ya wanawake kukaa vibarazani na kupiga stori, porojo pamoja na umbea huku vijana wa mtaa wakichagua maisha ya kuwa vibaka ili kupata vipato kwa njia fupi na nyepesi kwao na katika serikali ya mtaa ya kazamoyo wanashindwa kudhibiti vitendo hivyo na ndio maana wanakuwa mstari wa mbele kutetea maovu yanayoendelea dhidi ya vyombo vya dola.
MTAA WA KAZAMOYO Series imezalishwa na kampuni ya Cheni Arts Creation Company ltd na baadhi ya wasanii mashuhuri walioshiriki ni Mahsein Awadhi (Dr. Cheni), Amina Ahmed, Mwene Shina, Ester Darwesh, Elizabeth Chijumba, Queen Masanja, Hashim Kambi, Abdallah Mkumbila (Mzee Muhogo Mchungu) na wasanii wengi wameshiriki tamthilia hii na Itaanza kuruka tarehe 04 August 2023 kupitia channel 106 sinema zetu.
LORITA ni tamthilia inayotoa simulizi ya maisha ya vijana wa kisasa na namna wanavyokabiliana na changamoto za kimahusiano yaliyojaa usaliti, Tamthilia pia inatoa simulizi ya familia mbili zilizodhumiana pesa hivyo kila upande ukiapa kulipiza kisasi kwa mwenzake.
Tamthilia hii imeandaliwa na Magazijuto pictures chini ya muandaji William Mtitu pia wasanii walioshiriki pamoja na Angel Mazanda, Mariam Ismail, Christopher Mziwanda, Romeo George, Genevieve Mpangala, Denis David, Gysell Ngowi, Sadam Nawanda, Cojack chillo, Careen Simba, Jacqueline materu na wasanii wengi wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu. LORITA itaanza kuruka tarehe 14 August 2023 kupitia channel ya Sinema zetu.
Post a Comment