*Ifikapo Machi Jukwaa la Kiserikali (IGF) Kuendesha mafunzo kuhusu kodi za Madini*
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Augustine Olal, ametoa Vyeti kwa Wahitimu 28 wa Mafunzo ya Utunzaji Mazingira na kufunga migodi walioshiriki mafunzo hayo.
Amekabidhi vyeti hivyo leo Februari 23, 2024 katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Rafiki Hotel Jijini Dodoma.
Amesema dhumuni la mafunzo hayo lilikuwa ni kuongeza ujuzi, maendeleo na umahiri unaohitajika kwa utawala bora wa kijamii wa mazingira katika Uchimbaji Madini, ikisisitizwa juu ya kufungwa kwa Migodi na usimamizi wa mazingira.
Olal amesema, katika siku nne za mafunzo yalijikita katika mada muhimu kama vile Chombo na majibu ya maandalizi ya Dharura, Usimamizi wa maji, Udhibiti wa taka, Ufungaji wa Migodi na Uchimbaji baada ya uchimbaji.
Aidha, Olal amesema, Wizara iko tayari kushirikiana na Jukwaa la Kiserikali (IGF) katika kuwajengea uwezo watanzania katika sekta ya Madini na miradi mingine ambayo ni muhimu kwenye Wizara ya Madini na Sekta ya Madini kwa ujumla.
“Tunapohitimisha mafunzo haya, tuendeleze maarifa na uzoefu uliopatikana ili kuchangia maendeleo endelevu ya sekta yetu ya Madini na uhifadhi wa hazina zetu za asili zikiwemo juhudi zetu zifungue njia kwa wingi zaidi katika uchimbaji Madini unaozingatia mazingira na uwajibikaji nchini Tanzania,” amesema Olal.
Awali, Kamishna wa Madini Dkt. AbdulRahman Mwanga, amewashukuru na kuwapongeza wakufunzi kwa kutoa mafunzo stahiki na kuwashukuru washiriki wote kwa kushiriki kikamilifu na kusisitiza kuwa mafunzo haya yawe endelevu ili kuongeza wataalam katika tasnia hii ya Madini.
Post a Comment