Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania SMAUJATA wameungana na Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Mhe RC Albert John Chalamila kwa Kuwakemea Vikali wanaosema Madada Poa na Makaka Poa waradhalilshwa ama kanyang'anywahaki zao.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Katika Ukumbi wa Anatolgo Jijini Dar es salaam Mkuu wa Idara ya Maadili, nidhamu na Uongozi Taifa SUMAUJATA Fredrick Rwegasira amesema wanaendelea kukemea Tabia na Vitendo vinayoashiria mmomonyoko wa Maadili Kwa kuungana na Viongozi mbalimbali.
"Hakuna aligewadhalisha bali, Wamejidhalilisha wenyewe na haki yoyote inayohatarisha kesho yetu haifai kutazamva kama haki tena" amesema Rwegasira
Ameongeza kuwa Hahaweza Kuwatetea Watu wazima waloshindwa Kujitambua kwa Kuchagua kazi na Vitendo Vinavyohatarisha Kesho ya Watoto wa Afrika na hasa Tanzania ambao leo hawajui jema na baya.
"Haiwezekani Kubariki Vitendo hivi viovu, na Kama tumedhamiria kulinda Maadili yetu, basi tutambue anachokifanya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Hassan Bomboko ni Kupambana na Mlango au Chanzo kimojawapo cha Mmomonyoko wn Maadili" amesema Rwegasira.
Nae Wakili Katibu wa Idara ya Sheria Taifa SUMAUJATA Aristorko Msongela ameeleza vifungu vya adhabu na Sheria mbalimbali zinazotokana na Vitendo vya mmomonyoko wa Maduili ambopo kifungu cha 146 cha kanuni adhabu kimekataza na atakuwa amefanya makosa.
"Sisi kama Smaujata kitengo cha sheria tutaliomba bunge liongezee makali kanuni ya adhabu ya vifungu vya sheria"amesema msongela
Kwa Upande wake Mkuu wa Idara ya Itifaki Taifa SUMAUJATA Ridhiwani Maulidi amewaomba Vijana kushirikina na Serikali katika kuibua Watu wanaojihusisha na Vitendo vya mmomonyoko wa Maadili.
Hata hivyo Mwenyekiti wa SUMAUJATA Wilaya ya Ubongo Fatma Kivugo amesema Biashara ya Ushiga na Ukahaba zinapelekea kuleta athari mbalimbali katika Jamii ikiwemo ongezeko la Watoto wa mitaani.
Post a Comment