WAZAZI na walezi nchini wameshauriwa kujiunga na ADABIMA inayotolewa na Benk ya Biashara nchini(TCB) ili kuwawekea mazingira mazuri watoto wao kwenye safari ya Elimu.
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa kitengo cha Bima Benki ya TCB,Francis Kaaya,amesema Benki hiyo wameshirikiana na Metro life insurance wamekuja na ADABIMA.
"Tunatambua umuhimu mkubwa wa elimu katika kujenga kesho bora ya jamii yetu"Amesema.
Aidha,Kaaya amefafanua ADABIMA inatoa msaada pale mzazi anatakapopata majanga pia itaweza kumghalamia mtoto mpaka atakamaliza Elimu yake.
"Ikitokea kwa bahati mbaya Mzazi ametangulia mbele ya haki au kupata ulemavu wa kudumu basi ADABIMA itahakikisha mtoto anaendelea Kusoma."Amesema Kaaya.
Hata hivyo,Kaaya amesema pia ADABIMA itamsadia mtoto hata pale Ada za shule zitakapopanda pamoja na kufanyiwa uhamisho itahakikisha inaendelea kusimia uamisho ule.
"pia katika ADAMA pia tunatoa Milioni moja kwa mwaka kwa mwanafuzi kama pesa ya kujikimu"Amesema Kaaya.
Sanjari na hayo,Kaaya amewataka wananchi kutembele Banda la TCB Bank lilopo katika maonesho ya sabasaba kwa ajili kufungua Akaunti pamoja na kujipatia mikopo .
Kwa Upande wake,Mkuu wa Kitengo cha uendeshaji wa Bidhaa za kidigitali,Pray Henry Matiri,amewataka watanzania kujiunga huduma kikoba nakubainisha kuwa huduma hiyo ni zaidi ya fursa ya kidigitali inabeba dhana ya uwazi.
"Usalama katika uwekaji wa akiba na usimamizi bora wa kifedha tukitumia nyezo hii ya teknolojia,tunaviwezesha vikundi nchini kusimamia mategemeo yao kiuchumi,kukua kiuchumi na kujitegemea"Amesema Matiri.
Post a Comment