SHEKH SWED AWAJIA JUU WAPOTOSHAJI KWENYE MITANDAO

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Uzazi na Malezi Tanzania (UMATI)   Shekh Swed Twaib Swed akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam akikanusha taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zinazomkashifu na kumdhihaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluh Hassan na Chama cha Mapinduzi CCM ikionekana kuwa na sahihi yake kama  Mwenyekiki wa Bodi ya UMATI.

................

NA MUSSA KHALID

Chama cha Uzazi na Malezi Tanzania (UMATI) kimesikitishwa na kukanusha kuandaa taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zinazomkashifu na kumdhihaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluh Hassan na Chama cha Mapinduzi CCM.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Taifa UMATI  Shekh Swed Twaib Swed wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa taarifa hiyo iliyosambaa inaonekana kuwa na sahihi yake kama  Mwenyekiki wa Bodi ya UMATI jambo ambalo hakuwahi  kufikiria au kutenda kitendo hicho.

Mwenyekiti huyo ametumia fursa hiyo kuwaondoa hofu wananchama,Wabia,Wafanyaklazi na yeyote mwenye nia njeam na Shirika la UMATI kuhusiana na nyaraka hiyo ovu.

‘Ukweli ni kwamba nina kanusha kuhusika na kuandaa barua hii,lakini pia sijawahi na sitowahi kufikiria na au kuenda kitendo kama hiki kilichoandikwa kwenye barua hii na kwamba saini yangu ineghushiwa na sikushiriki kwa namna yeyote ile kuandaa na kusambaza karatasi hii’amesema Shekh Swed

Kuhusu  waliotajwa kwenye barua hiyo zikiwemo taasisi Mwenyekiti huyo amesema kuwa hakuna aliyehusishwa wala kuhusiaka kama karatasi linavyosema kwani jambo lenyewe halikuwa kutokea bali ni uzushi wa watu wenye nia ovu ya kuchafuana kupitia mitandao.

Aidha ameendelea kusisitiza kuwa kitendo kilichofanywa ni kibaya kutokana na  watu wenye nia ovu kumchonganisha na Mkuu wa Nchi, Chama cha Uzazi na Malezi Tanzania (UMATI) pamoja na Kiongozi Mkuu wa Dini ya Kiislamu Muft na Shekh Mkuu wa Tanzania Dkt Abubakari Zubeir sambamba na viongozi wengine.

‘Kwa kuwa jambo hili na dhihaka hizi zimesambazwa kupitia jina langu ingawa sihusiki kwa namna yeyote ile,ninatumia nafasi hii kumuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluh Hassan na serikali yetu tukufu’ameendelea kusisitiza Swed

Hata hivyo Mwenyekiti huyo amewataka wote wanaotumia mitandao ya kijamii kuhakikisha wanaitumia katika kujenga na kuelimisha watu sambamba na kufata taratibu na miongozo ya kimtandao ili kuepukana na mafarakano na taharuki katika jamii.

0/Post a Comment/Comments