WAOMBAJI 16,646 WACHAGULIWA KUJIUNGA NA VYUO

Mkurugenzi wa Udahili na Utunuku(NACTVET)Dkt Mercelina Bailtiwake,akizungumza na waandishi wa habari  Dar es salaam.
         ********

Na Mwandishi Wetu

 BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi(NACTVET)limesema jumla ya Waombaji 16,646 wamechaguliwa kujiunga na vyuo 221 vinavyotoa pogramu za Afya na Sayansi shirikishi ambapo wanawake 8,821 sawa na Asilimia 53 na wanaume 7,825 sawa na asilimia 47.

Akizungumzia na Waandishi wa Habari mapema jana Jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa Udahili na Utunuku(NACTVET)Dkt Mercelina Bailtiwake,amesema  jumla ya waombaji 24,629 waliwasilisha maombi yao kupitia mfumo wa udahili pamoja (CAS).

"Waombaji 23,503 walikamilisha maombi yao kwa kuchagua vyuo/pogramu walizozipenda,Waombaji 21,661 walikuwa na sifa kwenye pogramu walizoomba na waombaji 1,842 hawakuwa na Sifa kwenye pogramu walizoomba"Amesema

Hata hivyo,Dkt Bailtiwake,amesema Waombaji wenye sifa ambao hawakuchaguliwa kutokana na ushindani katika Programu na vyuo walivyoomba wanashauriwa kuomba kujiunga katika Programu na vyuo vyenye nafasi katika dirisha la awamu ya pili kupitia mfumo wa Udahili wa pamoja.

Dkt Bailtiwake, amewataka pia waombaji wote wanaweza kuangalia matokeo ya uchaguzi kupitia tovuti ya Baraza www.nactvet.go.tz kwa kubonyeza CAS selection 2024 kwa ajili ya kupata taarifa zaidi.

"Baraza linautaarifu Umma kuwa dirisha la awamu ya pili limefunguliwa Rasmi leo tarehe 11/07/2024 na litakuwa wazi hadi tarehe 10/08/2024,matokeo ya Uchaguzi yatatolewa tarehe 16/08/2024"


Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Mkurugenzi wa Udahili na Utunuku wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Dkt Mercelina Bailtiwake.


0/Post a Comment/Comments