******
Naibu Kamishina wa Kamisheni ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(TAHLISO) Lucy Mwamunda, amewaasa wanafunzi waliopata fursa ya masomo nje ya nchi, kuitumia nafasi hiyo kikamilifu kwa lengo la kuliletea Taifa manufaa.
Ametoa Rai hiyo Jijini Dar es Salaam katika sherehe fupi ya kuwaaga wanafunzi 19 waliopata fursa ya kwenda masomoni nchini Urusi kupitia Umoja ujulikanao kama "Youth Connectivity Gala", tukio lililoandaliwa na mtanzania anayesoma nchini humo Dorcas Mshiu.
Amesema Tanzania imefikia katika hatua ambayo elimu inaitazamwa kwa upana zaidi kiasi kwamba haitoshi kuwa elimu hiyo pekee bali elimu yenye viwango vya kimataifa hivyo ni vyema fursa za masomo zinazopatikana zikatumika ipasavyo kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
"Serikali inajitahidi kuboresha kiwango cha elimu nchini kuwa cha kimataifa na ndio maana tuna wanafunzi kutoka nje ya nchi wanaokuja kupata elimu Tanzania, hivyo nasi kama ilivyo kwa wao ni vyema wanafunzi wa kitanzania kupata elimu zaidi nje nchi ili kuongeza ushindani uliopo kimataifa na kuwa na uwezo wa kushindana nao" Amesema Lucy
Aidha Naibu huyo Kamishina wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa kwa niaba ya Tahliso, amempongeza Dorcas Mshiu kama mnufaika wa ufadhili wa masomo nchini Urusi kwa kuona fursa za masomo zilizopo nchini humo na kuitumia kuja kuwanufahisha wenzake waliopo nchini.
" TAHLISO chini ya Rais wetu Zainab Kitima, tunawaasa vijana 19 waliopata nafasi hii, tunatazimia wao kua chachu ya mabadiliko tunawaomba katika kila watakachokifanya fikra zao zote ziwe nyumbani kwa vijana wengi waliopo Tanzania ili kuona ni namna gani nao wataweza kunufaika na fursa zilizopo nchini humo na sehemu zingine" alisisitiza Lucy.
Ameongeza kuwa kama wao wanafunzi 19 wameshikwa mkono na mtu mmoja wao pia wanaweza kuwashika mkono vijana zaidi ya 19 na hivyo kusaidia Serikali katika jitihada za kuikuza elimu nchini lakini pia kusaidia vijana husika huku wakipaswa kuwa nafasi hiyo kwao waichukulie kama deni na siyo fursa.
Tukio la kuwaaga wanafunzi hao liliongozwa na Karibu wa Idara ya Uhusiano Kimataifa Vyuo Vikuu UVCCM Taifa Emmanuel Martine akimwakilisha Karibu Mkuu wa UVCCM Taifa Jokate Mwegelo sambamba na Dorcas Mshiu ambaye ndiye aliyewezesha fursa kwa wanafunzi hao.
Ends
Post a Comment