SERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TAASISI BINAFSI ZA ELIMU-KAPINGA

*****

Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema Serikali itaendelea kuwaunga mkono na kushirikiana na wadau wote wa elimu nchini ili kutimiza lengo la kufikisha elimu stahiki kwa makundi yote ya wananchi mijini na vijijini.

Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Agosti 17, 2024 wakati wa Maadhimisho ya Miaka 25 ya kusajiliwa kwa Shule ya Msingi Huruma inayomilikiwa na Kanisa Katoliki wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.

"Uwepo wa shule kama hii unadhihirisha jinsi mnavyoiunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita katika kutoa elimu bora kwa watanzania, nitumie fursa hii kulipongeza Kanisa Katoliki kwa kuendelea kuwa mdau mkubwa wa Serikali katika huduma za kijamii kama afya, elimu na huduma nyinginezo." Amesema Kapinga

Kuhusu shule hiyo ya Hekima amesema kuwa, Serikali inatambua mchango wa shule hiyo hasa kwa kutoa huduma kwa watoto wenye mahitaji maalum.

Mhe. Kapinga pia amewaasa Wanafunzi kuwa waaminifu pamoja na kujitolea katika kusaidia wengine.





 

0/Post a Comment/Comments