TAWIDO YAWAOMBA WADAU MBALIMBALI KUUNGANISHA NGUVU ILI KUDHIBITI SERIKALI VITENDO VYA KIKATILI

...............

Na Magrethy Katengu--Dar es salaam

Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia wanawake, wasichana na watoto Tanzania Women Initiative for development organization ( TAWIDO)  limetoa wito kwa Mamlaka za kiserikali na zisizo za kiserikali ikiwemo Polisi, Mahakama na bunge viongozi wa dini, familia,pamoja na vyombo vya habari  kuunganisha  nguvu ya pamoja ilikusaidia  kudhibiti vitendo vya ukatili nchini 

Wito huo ameutoa leo Agosti 21, 2024 Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Tawido Sophia Lugilahe ambapo amesema bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ni budi kufanya maboresho ya sheria ili kuipa nguvu sheria ya ukatili na unyasasaji wa kijinsi kwa watoto na wanawake na wanaume

Hata hivyo Mkurugenzi ameiomba serikali  kutenga bajeti ya kushughulikia vitendo vya kikatili ili kutoa nafasi kwa watumishi wa ustawi wa Jamii kuwa na fungu la kufutilia vitendo hivyo kwani  wakati mwingine watumishi wa ustawi wa Jamii wanapopewa taarifa za vitendo vya kikatili wanashindwa kufuatilia kwa wakati kutokana na kutokuwa na fedha,hali ambayo inasababisha kuzorotesha harakati za kudhibiti vitendo vya ukatili  kwa Jamii.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo wa TAWIDO ametoa wito kwa   Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya Marekebisho ya Sheria ili kudhibiti vitendo vya ukatili vinavyoendelea kushamili kwenye jamii.

Pia  Mahakama  imeshauriwa kumaliza kesi za ukatili kwa haraka na kutenda haki kwa watakaokutwa na hatia, hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao ili iwe fundisho kwa wengine wanaotenda makosa kama hayo.

"Jamii kwa ujumla inatakiwa kuungana ili kufichua vitendo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria watuhumiwa wanaojihusisha na vitendo vya Ukatili"amesema Mkurugenzi 

Aidha amewakumbusha  wazazi kuacha  kukwepa majukumu ya kulea watoto wao kwa maana ujenzi wa tabia  njema inaanza kujengwa kwenye malezi na kuwapa ulinzi.

Amesema kuwa katika ofisi ya TAWIDO kuna kituo cha kupokea taarifa za kikatili kupitia simu (Call centre) ambapo tangu mwaka 2021 hadi  mwaka huu wameweza kupokea taarifa za vitendo vya ukatili takribani 38, 238.

Katika takwimu hizo, wanawake ni 27,828 wanaume 9352 na watoto ni 9038 na kuweka wazi taarifa hizo ni kwa wale wanofahamu namba ya kituoni hapo.

Amesema kuwa takwimu hizo zinaonesha jamii haiko salama Jambo ambalo litasababisha  kutokuwepo kwa maendeleo kutokana na uwezo wa kundi la watoto waliolawitiwa ama kubakwa , hivyo hatua za haraka zinatakiwa kuchukuliwa kudhibiti hayo.

Pia amesema katika kipindi hicho ukatili wa kimwili zilikuwa na matukio 12,243 huku ukatili wa kijinsia ukiwa 7403, wa kingono ukiwa 13,216 wa kiuchumi ukiwa 3,375 na watoto ni 938.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Madereva wa Bodaboda na Bajaji Mbezi Beach Tumainieli Elisha amewataka maafisa usafirishaji hao kuhakikisha wanatoa taarifa pindi wanapoona kuna viashiria vya vitendo vya ukatili kwenye maeneo yao ya kazi.

"Tuwe na tabia ya kutoa elimu kwa abiria wetu watende mema, tukifanya hivyo kwa ushirikiano tutafanikiwa, hata vitendo vinavyofanywa na wafanyakazi wa ndani wakati mwingine vinachochewa waajiri wao,tabia ya kuwacheleweshea mishahara,kuwabagua hata wakati wa chakula nahuku wao ndio walinzi wakubwa wa familia wakati tukiwa kazini,hivyo wanafikia hatua wanachukua uamzi mgumu hata wa kuwadhulu watoto nyumbani"amesema Elisha.

0/Post a Comment/Comments