********
Kicheko kimetawala kwa wananchi Kijiji cha Lwinga wilayani amtumbo, Ruvuma baada ya Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kutangaza kurejesha hekta 3000 kati ya hekta 6,580 za shamba la Serikali kwa wakulima.
Bashe amesema anatambua kuwa shamba hilo lina siasa nyingi lakini ni lazima kufanya maamuzi magumu kwa maslahi ya wananchi ambao wana haki ya kumiliki shamba hilo.
Akizungumza wilayani humo katika muendelezo wa ziara yake alisema, wananchi wa kijiji cha Lwinga wilayani Namtumbo wana haki ya kumiliki shamba hilo.
“Iwapo kuna mwenye hoja awasiliane na mimi haiwezekani wananchi hawa wakose maeneo na wachache watake kujimilikisha wanavyotaka wao.
Alisena shamba hilo lilikuwa la wananchi wakalitoa kwa Serikali chini ya NAFCO ambao walilitumia kwa miaka nane kisha kulitelekeza na baadaye kurudishwa Wizara ya Kilimo na kisha wao kulitoa kwa Wakala wa mbegu ASA. Hata hivyo, Waziri Bashe alisema shamba hilo limekuwa katika mgogoro kwa zaidi ya miaka 20 huku wananchi wakiwa hawana ardhi ya kilimo.
"Mimi ndio Waziri wa Kilimo nilishatoa maamuzi nasisitiza ekari 3,000 wapewe wananchi na ekari 3,580 zitengwe kwa ajili ya mbegu
“Watu hawa ni waungwana sana si busara wananchi ambao walijitolea ardhi yao kuwa watumwa nafahamu wapo wachache wanaotaka kujimilisha na kuwafanya wenye haki kuwa manamba,”alisisitiza.
Alissna haoni haja ya kuwapo kwa mgogoro katika ardhi hiyo kwani wanufaika wa mbegu zinazokwenda kuzalishwa ndio hao wakulima.
Mbunge wa jimbo hilo, Vita Kawawa aliishukuru Serikali kwa kazi kubwa inayofanya sekta ya kilimo hususani katika utoaji wa ruzuku za pembejo.
Post a Comment