NCCR Mageuzi YATUMA SALAMU ZA POLE KWA CHAMA CHA CHADEMA

Mwenyekiti Taifa wa Chama cha siasa cha NCCR Mageuzi Haji Ambar Khamis (picha na mtandao)
................. 

NA MUSSA KHALID

Mwenyekiti Taifa wa Chama cha siasa cha NCCR Mageuzi Haji Ambar Khamis ametuma salamu za Pole kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kufuatia kufariki kwa kiongozi wao Ali Kibao katika mazingira ya utata.


Pia Mwenyekiti huyo amesema ni vyema watu wakasubiri taarifa kutoka Jeshi la Polisi kutokana na wao ndio wenye kufanya uchuguzi ili kubaini chanzo cha kifo chake na kama kuna wahusika waweze kuchukuliwa hatua stahiki.


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Mwenyekiti huyo amesema kutokana msiba huo kukaa kisiasa  amesema kwa sababu wanasiasa sio wachunguzi hawawezi kusema kifo hicho kimesababishwa na kitu gani hivyo ni vyema wakawa watulivu katika wakati hu mgumu.


' Sisi tunaweza kusema kwamba Bwana ametoa Bwana ametwaa Jina lla Bwan  lihimidiwe kwa sababu yote ni kudra ya Mungu ,kwa mfano Tundu Lissu alipigwa risasi kumi na saba na hakufa lakini Abubakari Hamis Barakari wa ACT Wazalendo kule Zanzibar ilipita chini ya miguu tu risasi na haikumgusa akafa hivyo ni lazima tumkabidhi Mungu katika masuala kama hayo'amesema Mwenyekiti Haji


Katika Hatua nyingine ,kuelekea nyakati za uchaguzi Mwenyekiti huyo amesema ni vyema Jeshi la Polisi likashirikiana na wananchi kwa ajili ya kuzuiya uhalifu na wanapopata taarifa wanapaswa kuwajuza wananchi kwa haraka.


'Kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na Mkuu mwakani ili jambo hili likomeshwe ni lazima Polisi wafanyekazi kwa juhudi na maarifa na wanaohusika wachukuliwe hatua bila ya kupepesa macho ili kutoharibu taratibu za kinchi huko baadae'ameendelea Kusisitiza Mwenyekiti NCCR Mageuzi Haji


Kwa mujibu wa Taarifa ambayo imetolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi DCP David Misime imesema Jeshi hilo lilipokea taarifa na kuanza uchunguzi wa kubaini kilichotokea,chanzo chake na watu waliohusika ni akina nani.

Picha ya mjumbe wa Sekretarieti ya Chadema ambaye anadaiwa jioni ya Septemba 6, 2024 maeneo ya Kibo Complex Tegeta jijini Dar es Salaam, akiwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea Tanga akiwa kwenye basi la Tashrif alishushwa kwenye basi hilo na kuchukuliwa na watu wasiojulikana majina yao wala walipotokea.

0/Post a Comment/Comments