Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani Kanal Joseph Kolombo akizungumza wakati akifungua warsha ya mafunzo maalum ya siku mbili Oktoba 21-22,2024 kwa vikundi vya ufugaji nyuki,upandaji mikoko na Utalii wa Ikolojia katika delta ya mto Rufiji ambayo imeandaliwa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la PAKAYA Culture Environmental Groups (PCEG) na inafanyika katika ukumbi wa chama cha Walimu (CWT) Kibiti Mkoani Pwani.
Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la PAKAYA Culture Environmental Groups (PCEG) Abdallah Ally Pendekezi akizungumza akieleza dhamira ya kuandaa warsha ya mafunzo maalum ya siku mbili Oktoba 21-22,2024 kwa vikundi vya ufugaji nyuki,upandaji mikoko na Utalii wa Ikolojia katika delta ya mto Rufiji na inafanyika katika ukumbi wa chama cha Walimu (CWT) Kibiti Mkoani Pwani.
Baadhi ya wanavikundi vya ujasiriamali ambao wameshiriki katika warsha ya mafunzo maalum ya siku mbili Oktoba 21-22,2024 kwa vikundi vya ufugaji nyuki,upandaji mikoko na Utalii wa Ikolojia katika delta ya mto Rufiji ambayo imeandaliwa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la PAKAYA Culture Environmental Groups (PCEG) na inafanyika katika ukumbi wa chama cha Walimu (CWT) Kibiti Mkoani Pwani.
Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la PAKAYA Culture Environmental Groups (PCEG) Abdallah Ally Pendekezi (wa pili kulia) sambamba na Mkurugenzi wa Mipango na uchumi wa Shirika la Pakaya Culture Environment Groups Bakari Hassan Kisoma (wa kwanza kushoto) wakionyesha Tenti litakalotumika kwa ajili ya Utalii wa Ikolojia
Picha ya pamoja ya Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani Kanal Joseph Kolombo akiwa pamoja na viongozi wa PAKAYA na vikundi vya ufugaji nyuki,upandaji mikoko na Utalii wa Ikolojia katika delta ya mto Rufiji katika warsha ya mafunzo maalum ya siku mbili Oktoba 21-22,2024 ambayo imeandaliwa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la PAKAYA Culture Environmental Groups (PCEG) na inafanyika katika ukumbi wa chama cha Walimu (CWT) Kibiti Mkoani Pwani.
..........................
NA MUSSA KHALID,KIBITI PWANI
Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani Kanal Joseph Kolombo amesema kuwa serikali inaendelea kuhakikisha inaliunga mkono Shirika lisilokuwa la Kiserikali la PAKAYA Culture Environmental Groups (PCEG) katika uhifadhi na upandaji wa mikoko ikiwemo kuweka mkazo wa kuzuia shughuli za kibinadamu ili kutoathiri mazingira.
Mkuu wa Wilaya Kanal Kolombo amesema hayo leo Wilayani Kibiti Mkoani Pwania wakati akifungua warsha ya mafunzo maalum ya siku mbili kwa vikundi vya ufugaji nyuki,upandaji mikoko na Utalii wa Ikolojia katika delta ya mto Rufiji ambayo imeandaliwa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la PAKAYA Culture Environmental Groups (PCEG).
DC Kanal Kolombo amesema ni vyema wananchi wakashirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la PAKAYA katika Kudhibiti uharibifu wa mikoko badala yake iendelee kutokea Elimu ya uhifadhi.
"Ninawaomba PAKAYA kuendelea na jitihada hizo kwa kuwa na malengo makubwa na tuyatekeleza mfano haya ya ufugaji wa nyuki tunaweza pia kugawa mizinga katika baadhi ya vijiji kwa kipindi Fulani au tutapanda mikoko jambo ambalo litafanya uimara wa uhifadhi na urutubishaji wa mikoko hiyo"amesema DC Kanal
Amesema juhudi za serikali inakwenda sambamba na mashirika mbalimbali lakini pia inahakikisha wanawasimamia wananchi kupunguza shughuli za kibinadamu katika delta ya Mto rufiji ikiwemo kulima na kukata mikoko jambo ambalo imeamua kuwapa kazi mbadala kwa kuwapa boti na kuwapatia mizinga ya nyuki ili kuongeza uchumi.
Awali akizungumza Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la PAKAYA Culture Environmental Groups (PCEG) Abdallah Ally Pendekezi amesema dhamira yao ni kuendelea kuhakikisha wanahamasisha uhifadhi shirikishi wa Mazingira ikiwemo upandaji wa mikoko ili jamii iweze kufahamu namna ya kuyatunza.
“Kimsingi sisi wana PAKAYA kazi yetu ni kuendelea kuwawezesha wananchi wanajamii waliopo katika maeneo mbalimbali kutumia rasilimali asilia ili waweze kunufaika nazo”amesema Pendekezi
Kuhusu ufugaji wa nyuki,Mwenyekiti Pendekezi amesema kwa awamu hii katika mradi huu wamenunua zaidi ya mizinga 20 hivyo wanaangalia eneo stahiki ambalo itawekwa baada ya kupanda mikoko.
‘Kwa kawaida ilikuwa hatuwezi kugawa iwe mizinga au vifaa vinginevyo ikiwemo miti tumekusudia kuhifadhi mazingira na ndio maana tumeanzisha vikundi ili uwajengea uwezo’ameendelea kusisitiza Pendekezi
Aidha amewasisitiza wanavikundi vya ujasiriamali kuhakikisha wanazingatia yote wanayoelekezwa na kwenda kufanyia kazi maagizo waliyopewa kwani ni kwaajili ya kuwanufaisha kwa ustawi wa mtu mmoja mmoja au hata vikundi.
Kwa upande wao baaadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Sadah Shabani kutoka kijiji cha Nyamisati na amesema kuwa yatawajengea uwezo wa kuweza kuanzisha vituo vya utalii katika maeneo yao kutokana na kuwa na fursa kubwa zikiwemo fukwe zilizopo huku Rasul Omary msaidizi misitu akisema manufaa ya utunzaji mikoko inasaidia katika maeneo mbalimbali ya kibinadamu.
Post a Comment