MPOGOLO AWATAKA WATALAMU UJENZI KUSHIRIKIANA.


.................. 

Timothy Marko

MKUU wa Wilaya ya ilala Edward Mpogolo amewataka Wabunifu Majenzi na Ukadiriaji Majengo kuweza kushirikiana katika utendaji wa kazi zao nasio kukosoana pindi panapotokea Changamoto za Majenzi katika Sekta hiyo. 

Akimwakilisha Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko katika Maafali ya Wahitimu wa Kada hiyo Jijini Dar es Salaam Edward Mpogolo amesema kuwa SERIKALI inaendelea kuboresha Sheria ya Manunuzi katika Sekta ya ujenzi nakuwataka watalamu kushirikiana ilikondokana na Utegemezi wa watalamu hao kutoka Nje katika Miradi Mbalimbali inayoendelea hapa Nchini.

"Tasisi za kusimamia Majenzi zinawajibu Mkubwa wakuhakikisha Watalamu wanazingatia Sheria"Alisema Mkuu wa Wilaya ya ilala Edward Mpogolo.

 

Mpogolo akimwakilisha Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko Aliongeza kuwa Watalamu Wengi wamajenzi Baadhi yao hubadilika na kusahau Maadili Yao Baada ya kuhitimu Mafunzo Yao.

Aliwataka Watendaji wa SERIKALI kusimamiana na kuthaminiana katika Utendaji wa Majukumu Yao .

"Wilaya ya ilala tunamasoko lakini kumekuwa na Changamoto za Masoko kumekuwa na Michoro sio Rafiki kwa Wafanyabiashara"Alisisitiza Edward Mpogolo.


Kwa upande wake Msajli wa Majenzi wa Bodi ya QRB Mhandisi John Mduma amesema kuwa Teknolojia ya Sekta ya ujenzi inakua kwa kasi.

Alisema kuwa Mpango wakuwawezesha wakandarasi wandani unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.

"Ujuzi uliotumika Katika Ujenzi wa Majengo wa ya kihistoria ya yameanzia wapi"Alisema Mhandisi John Mduma

 

0/Post a Comment/Comments