LEO ikiwa siku maalumu kwa wananchi wa Tanzania bara kupiga kura ili kuwachagua viongozi wao wa serikali ya mitaa,vijiji na vitongoji, Mkuu wa wilaya ya Chato,Louis Bura,ameungana na wananchi wa wilaya hiyo kupiga kura ili kutimiza takwa la kikatiba na haki yake kidemokrasia.
Mkuu huyo amefika kwenye kituo cha kupigia kura kwenye kijiji cha Rubambangwe, majira ya saa 2:2 asubuhi kabla ya kutembelea vituo mbalimbali ili kuona hali halisi ya ulinzi na usalama kwa wananchi waliojitokeza kushiriki katika zoezi hilo muhimu.
Wengine walioshiriki mchakato huo kwa nyakati tofauti ni Katibu tawala wa wilaya hiyo, Thomas Dimme, mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo,ambaye pia ni Mkurugenzi wa uchaguzi huo jimbo la Chato, Mandia Kihiyo.
Akizungumza na vyombo vya habari mkurugenzi wa Uchaguzi, amesema zoezi linakwenda vizuri na kwamba vifaa vimefika maeneo yote kwa wakati na kwamba zoezi hilo limeanza saa 2 asubuhi na litahitimishwa majira ya saa 10 jioni.
"Zoezi lina kwenda vizuri na tunatarajia aslimia 95 ya waliojiandikisha watapiga kura,na mpaka muda huu bado sijapokea malalamiko kutoka chama chochote cha siasa kilichoweka wagombea"amesema Kihiyo.
Amevitaja vyama vilivyosimamisha wagombea kwenye maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo kuwa ni Chama Chaapinduzi(CCM) Chama cha Demokrasia na maendeleo(Chadema) pamoja na ACT wazalendo.
Aidha amepongeza mwitikio wa wananchi wanavyojitokeza kwenye vituo vya kupiga kura na kwamba ni matumaini yake kuwa kila mwananchi atapata fursa ya kumchagua kiongozi anayemtaka pasipo kushurutishwa na mtu yeyote.
Akizungumzia zoezi hilo,mkuu wa wilaya hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama, amesema hali ya usalama kwa wananchi ipo vizuri na kwamba wananchi wanaendelea kupiga kura kwa amani na utulivu.
Amesisitiza kuwa kila mwananchi akimaliza kutimiza haki yake ya kupiga kura anapaswa kurudi nyumbani kwa utulivu ili kungoja matokeo yatakayotangazwa.
Hata hivyo amedai kuwa changamoto ndogondogo zilizojitokeza zimetatuliwa haraka kabla ya kuleta taharuki kwa wapiga kura na kwamba wananchi waendelee kujitokeza ili kuwachagua viongozi wao wanaofaa kuwatumikia.
Baadhi ya mawakala wa vyama vya siasa wamepongeza utaratibu wa kupiga kura kwa madai hakuna hujuma zinazoonekana kufanyika.
"Tunashukuru kituo chetu kimefunguliwa tangu saa 1:30 na tumeanza kupiga kura saa 2 asubuhi,kwa kweli mpaka sasa hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza "amesema wakala wa Chadema Magayane Ndyame.
Kwa upande wake Mariamu Juma,Wakala wa ACT wazalendo, amesema uchaguzi huo unaendelea vizuri na kwamba hakuna vitisho vyovyote,hivyo anaamini uchaguzi utakuwa huru na haki.
Bukwimba Mihambo,mkazi wa kijiji cha Matabe,anasema ametumia takribani dakika 4 kupiga kura kuchagua viongozi anao wahutaji.
Katibu tawala wilaya ya Chato,Thomas Dimme, akipiga kura.Wananchi wakiendelea kupiga kura
Post a Comment