MUHAS NA SWEDEN WASISAINI MKATABA WA USHIRIKIANO WA MIAKA SITA

 

Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Apolinary Kamuhabwa, kulia na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania, Charlotte Ozaki Macia ( katikati) wakisaini mikataba wa makubaliano ya kwa ajili ya kuimarisha utafiti wa uvumbuzi na mfumo kwa wanafunzi wa Uzamili na Uzamivu wenye thamani ya zaidi ya bilioni 12. Makubaliano hayo yameingiwa kati ya Shirika la Sida kutoka Swiden na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas) katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam leo Novemba 14,2024. Anayeshuhudia Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya chuo hicho, Prof. Harrison Mwakyembe.
xxxxxxxxxxxxxxx


Na Karama Kenyunko Michuzi Tv 
CHUO Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kwa kushirikiana na ubalozi wa Sweden nchini wamesaini mkataba wa makubaliano ya jsgirikiano wa a miaka sita yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 12 kwa ajili ya kuimarisha utafiti, uvumbuzi na mafunzo kwa wanafunzi wa shahada ya uzamili na uzamivu.

Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini makubaliano hayo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo Novemba 14, 2024 Makamu Mkuu wa MUHAS, Profesa Appolinary Kamuhabwa amesema utekelezaji wa makubaliano hayo utaanza rasmi mwezi Desemba mwaka huu na kuendelea hadi Juni 2030.

"Leo, tumetia saini mkataba mpya wenye thamani ya dola za Marekani milioni tano, ambao utaanza rasmi mwezi Desemba. Mkataba huu utaangazia maeneo makuu matatu, ambayo ni mafunzo, uvumbuzi na utafiti," amesema Profesa Kamuhabwa.

Ameongeza kuwa katika ushirikiano huo na MUHAS pia inashirikiana na vyuo vikuu vitatu vya Sweden, ikiwemo Umeå, Chuo Kikuu cha Uppsala na Taasisi ya Karolinska, ambapo huko watashiriki kama wasimamizi wa pamoja wa wanafunzi wa shahada ya uzamivu.

Hata hivyo, Profesa Kamuhabwa amesema Tanzania na Sweden zimekuwa zikishirikiana  kufanya tafiti kwa miaka 48 sasa huku Ushirikiano huo ukiwa umelenga kuongeza uwezo wa chuo hicho kushughulikia changamoto za kiafya kitaifa, kama vile rasilimali watu katika sekta ya afya, sera na miongozo ya afya na mabadiliko katika hali ya magonjwa.

"Awamu iliyopita ya msaada wa Sweden kwa kipindi cha 2015-2023, umeongeza idadi ya wanasayansi. Kati ya 2015-2024 umesaidia wanafunzi 32 wa shahada ya uzamivu (sawa na asilimia 86 ya waliosajiliwa), na wanafunzi 11 wa shahada ya uzamili (sawa na asilimia 69 ya waliosajiliwa) wamehitimu," alisema.

Hata hivyo, ameishukuru serikali ya Sweden kwa msaada wao, akisema msaada huo utawezesha taasisi hiyo kuendeleza suluhisho sekta ya afya.

Kwa upande wake,  Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Bi Charlotta Macias, amesema ubalozi unatarajia kushirikiana na MUHAS katika awamu mpya ambayo pia ni ya mwisho ya msaada wa Sweden kwa chuo hicho.

"Ubalozi ungependa kushirikiana na MUHAS na kuendelea kutangaza matokeo mazuri ya utafiti yaliyofikiwa. Pia tungependa kushirikiana na MUHAS kuhamasisha kuongezwa kwa ufadhili wa kitaifa kwa mafunzo ya juu ya utafiti," amesema. 

Balozi wa Sweden Nchini Tanzania, Charlotte Ozaki Macia  akizungumza kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano  kwa ajili ya kuimarisha utafiti wa uvumbuzi na mfumo kwa wanafunzi wa Uzamili na Uzamivu wenye thamani  ya zaidi ya  bilioni 12.  Makubaliano hayo yameingiwa kati ya Shirika la Sida kutoka Swiden na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas)  katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Muhas, Prof. Harrison Mwakyembe  akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba  makubaliano ya ushirikiano  kwa ajili ya kuimarisha utafiti wa uvumbuzi na mfumo kwa wanafunzi wa Uzamili na Uzamivu wenye thamani  ya zaidi ya  bilioni 12.  Makubaliano hayo yameingiwa kati ya Shirika la Sida kutoka Swiden na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas)  katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam
Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi  Shirikishi  Mhimbili (MUHAS), Apolinary Kamuhabwa(wa pili kulia) na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania, Charlotte Ozaki Macia ( wa pili kushoto) wakibadilishana nyaraka  baada ya  kusaini mkataba wa  Mashirikiano wenye  thamani  ya zaidi ya  bilioni 12.5 kati ya Swiden(Sida)  na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas)  katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi wa chuo hicho, Prof. Harrison Mwakyembe na Mshauri wa maswala ya utafiti wa ubalozi Sweden, Eva Ohlsson
Picha ya pamoja.

0/Post a Comment/Comments