Chama cha NLD kimesema
kitashiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika mikoa 10 nchini, huku
kikipongeza mchakato wa uchaguzi huo kwa kusema kuwa unaenda vizuri na umekuwa
ni wa ushirikishwaji.
Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa
NLD Doyo Hassan Doyo amesema mchakato wa uchaguzi umekuwa wa haki na unakwenda
na majadiliano ambapo vyama vyote 19 vilishiriki mkutano ulioandaliwa na Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Doyo amesema ni hatua kubwa katika siasa za nchi
kwa kuwa hakuna chama hata kimoja kilichosema hakitashiriki uchaguzi huo wa
Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27,2024.
Post a Comment