NA MUSSA KHALID
Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa
TAKUKURU Kinondoni imepokea Jumla ya Malalamiko 104,yaliyohusu rushwa
yakiwa 72 huku yasiyohusu Rushwa
yakiwa 32 katika kipindi cha mwezi Julai
hadi Septemba mwaka huu.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Kaimu
Mkuu wa Takukuru (M) Kinondoni Christian Nyakizee wakati akizungumza na
wanahabari akitoa taarifa ya majukumu waliyoyafanya kwa kipindi hicho.
Aidha Nyakinzee amesema kuwa katika kipindi hicho
pia wamefungua mashauri mapya mawili katika mahakama ya wilaya ya Ubungo,
ambapo mashauri saba yaliyolewa maamuzi na Jamhuri imeshinda mashauri matatu
huku 24 yakiwa yanaendelea mahakamani.
Kuhusu uzuiaji rushwa,amesema wamefuatili miradi
miradi sita yenye thamani ya Bill 15 ambayo imeendelea na utekelezaji ambapo
wamebaini mapungufu na wanaendelea kufuatilia mpaka itakapokamilika.
“Katika kipindi hicho pia tumefanikiwa kufungua mashauri mapya mawili (02) katika Mahakama ya Wilaya ya Ubungo, huku mashauri saba (7) yalitolewa maamuzi na Jamhuri imefanikiwa kushinda mashauri matatu (3) na mashauri 24 yanaendelea mahakamani”amesema Nyakinzee
Kaimu Mkuu huyo wa TAKUKURU Kinondoni amesema katika
uchambuzi wa mfumo ambao wamefanya
wamebaini kuwepo kwa changamoto katika utengenezaji wa Ankara unaotokana
na uwepo wa dira za maji ndani ya makazi ya wateja hivyo kupelekea
ucheleweshaji kwenye usomaji wa dira kwa kutofika kwa wakati.
Katika Hatua nyingine TAKUKURU Mkoa Kinondoni imejipanga kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa kuendelea kuelimisha wananchi wajue madhara ya rushwa na wahamasike kushirikiana na Taasisi hiyo kutokomeza Rushwa kuanzia sasa mpaka wakati wa uchaguzi.
Post a Comment