RC CHALAMILA AUNGANA NA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MZEE JOHN TUTUBA

.................

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Novemba 04, 2024 ameungana na mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa Mzee John Tutuba ambaye ni baba mzazi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Emmanuel Tutuba katika Kanisa Katoriki Parokia Joseph Mwenyeheri wa Allamano Kibada-Kigamboni

RC Chalamila katika tukio hilo aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt Toba Nguvila pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo.

Aidha Mzee Tutuba alifariki Novemba 01, 2024 katika Hospitali ya Shifaa Pan African ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam alipokuwa akitibiwa na anatarajiwa kuzikwa Wilaya ya Kibondo Mko wa Kigoma.

0/Post a Comment/Comments