WAZIRI wa fedha Dkt. Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi
katika Mahafali ya 17 ya Chuo cha Kodi (ITA) yatakayofanyika Novemba 22, 2024
jijini Dar es Salaam.
Pia Nchemba katika mahafali hayo atawatunuku vyeti Wahitimu wa vyeti,
Stashahada, Shahada na Stashahada ya Uzamili.
Hayo yamebainishwa Jana mapema jijini Dar es Salaam na mKuu wa Chuo cha Kodi
(ITA), Profesa Isaya Jairo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo
amesema “Pamoja na kutunuku vyeti pia atatoa zawadi kwa wanafunzi wanaobaki
chuoni hapa ili kuwapa moyo wa kuendelea kufanya vizuri katika masomo
yao.Katika idadi hiyo wanaume ni 236 na wanawake 181 ambapo195 watatunukiwa
cheti cha Uwakala wa forodha wa Afrika Mashariki(EACFF).” Amesema Jairo
Ameongeza,”Wahitimu 28 watatunukiwa Cheti cha Usimamizi wa Forodha na Kodi
(CCTM), 61 watatunukiwa Stashahada ya Usimamizi wa Forodha na kodi (DCTM), 119
watatunukiwa Shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi (BCTM) na Wahitimu 14
watatunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Kodi (PGDT).” Amesema Prof.Jairo.
Prof. Jairo amesema Chuo hicho kinajivunia mafanikio mengi katika utekelezaji
wa Mpango mkakati wa awamu ya Tano wa Chuo ambao umejikita katika kutoa mafunzo
kwa njia ya kisasa yaani kidijitali.
“Tayari maandalizi ya kutoa elimu masafa kwa njia ya mtandao yameanza na
yanaendelea vizuri hivyo itasaidia kupunguza gharama kwa wanafunzi walioko
mikoani na kuongeza idadi ya wahitimu kwani mwanafunzi hayakuwa na ulazima wa
kusafiri kuja chuo bali kila kitu atapata mtandaoni.” Amesema Prof.Jairo
Amesema pamoja na jukumu kubwa la kutoa mafunzo kwa watumishi wa TRA, Chuo cha
Kodi vilevile kinatoa mafunzo na ushauri elekezi kwa wadau wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania(TRA) na mamlaka zingine za Mapato Afrika kama vile Sudan, Botswana na
Somalia.
Prof. Jairo ametumia nafasi hiyo kuikumbusha jamii kuwa kufanyika kwa mahafali
ni fursa nzuri ya kuwapongeza wahitimu pamoja na kutathmini mafanikio na
shughuli ambazo zinafanywa na Chuo. Pamoja na kuwaalika wageni kutoka Mataifa
mbalimbali ambao ni wadau na washirika katika maendeleo ya taaluma ya forodha
na kodi ili kuvutia fursa za uwekezaji.
Post a Comment