...............
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema mashabiki wa timu ya CS SFAXIEN wamevunja viti 156 vya rangi ya buluu na 100 vya rangi ya orange, ambavyo viko katika uwanja wa benjamini mkapa.
Kupitia taarifa ya kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam, Jumanne Murilo imesema kuwa sababu ya kuvunjwa kwa viti hivyo ni mashabiki wa timu ya CS SFAXIEN kuonesha kutoridhika na maamuzi ya mwamuzi wa mchezo, hasa kutokana na kuongeza kwa dakika saba za nyongeza, jambo ambalo lilipelekea timu ya Simba kupata goli la pili na la ushindi.
Aidha katika vurugu hizo shabiki mmoja wa timu ya CS SFAXIEN aliumia na kupatiwa huduma ya kwanza na kuruhusiwa.
Hata hivyo Jeshi la Polisi limesisitiza kuwa litashirikiana na mamlaka zingine za kisheria na za soka kuchukua hatua kali dhidi ya vitendo vya fujo ambavyo ni kinyume na sheria na vinavunja utaratibu wa michezo.
Post a Comment