******
Na Mwandishi Wetu
Vodacom imesema inaendelea kuboresha maisha ya watu kupitia teknolojia na huduma za kijamii hasa kwa kujenga minara vijijini.
Akizungumza Mwishoni Mwa Wiki katika
Mkutano wa Chakula cha Jioni cha Viongozi Wakuu wa Kampuni, Mkurugenzi wa Fedha
katika Kampuni ya Vodacom Tanzania, Hilda Bujiku, alisema wanataka kupanua
mtandao wa mawasiliano kwa maeneo ya mbali, ambayo mara nyingi hukosa huduma za
msingi za mawasiliano.
Aidha, alisema Vodacom imeonyesha
dhamira yake ya kusaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuweka lengo
la kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa (carbon emissions) na kufikia hali ya
kutokuwa na uzalishaji wa kaboni (net zero emissions) ifikapo mwaka 2035.
Pia, alisema kampuni hiyo ya Vodacom
kupitia Programu yake ya E-Fahamu wanaendelea na juhudi za kuhakikisha
wanawekeza katika elimu kwa kutumia teknolojia ya kidijitali, ambapo programu
hii inaweza kusaidia kupunguza pengo la maarifa kwa kuwezesha upatikanaji wa
rasilimali za kielimu kwa njia rahisi na nafuu.
Kuhusu tuzo waliyoipata katika kongamano hilo, ambayo inawatambua kama mshirika mkuu ambaye ameendelea kuonesha na kuongoza katika maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi, Bujiku alisema tuzo hiyo inawapa chachu zaidi ya kuendelea kufanya shughuli za kila siku kwa maendeleo ya kiuchumi.
Post a Comment