Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati
Dkt. Biteko amesema hayo leo Desemba 17, 2024 wakati akifungua Kongamano la 15 la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi linaloendelea Jijini Arusha.
asilimia 70 ya bajeti nzima ni kwa ajili ya manunuzi, hivyo
kuweni waadilifu, Chukieni Rushwa na kushauri namna bora ya kufanikisha mipango
ya Maendeleo” amesema Dkt. Biteko.
Hata hivyo, Dkt. Biteko amewataka washiriki wa Kongamano hilo kujifanyia tathimini kuhusu utendaji wao wa kazi ili kuondokana na Changamoto zinazoweza kuichafua taaluma ya ununuzi na ugavi.
“ Zipo sauti nanyi mnazisikia, ili uweze kupata tenda lazima
kuwa na urafiki na Afisa ununuzi, wanasema ukifuata taratibu za ununuzi gharama
zinaongezeka zaidi ya kawaida, wengine wanasema siri za tenda zinapatikana
miongoni mwa watumishi, wengine wanalaumu na wengine wanasifia, Jambo la msingi
sikilizeni sauti za watu na mjitathimini,” amesisitiza
Amesema miongoni mwa mambo yanayosababisha mkwamo Serikalini ni pamoja na Wivu, choyo na fitna miongoni mwa watumishi, hivyo amewataka kuondokana na mambo hayo ili kukua na kujiletea maendeleo.
“Sheria ya ununuzi wa umma sura 410 inawalinda wataalam wa
ununuzi na ugavi hivyo watembee kifua mbele na kuhakikisha wanafanya kazi kwa
mujibu wa sheria zilizopo”.
Amesema Bodi hiyo inaendelea na utekelezaji wa Sheria Na. 23
ya mwaka 2007 kuhakikisha kuhakikisha Wataalam wanaofanya shughuli za ununuzi
na ugavi wana sifa stahiki za kufanya kazi hizo.
Post a Comment